Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Utakaso ni Nini?

  Mafundisho mapotofu kuhusu utakaso hutokana na kutojali na kukataa kutii sheria ya Mungu. Upotofu huu wa mafundisho ya uongo na ya hatari kubwa hupendelewa na watu wengi.TU 226.5

  Paulo asema “maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kutakaswa kwenu” Biblia hufundisha dhahiri kuwa utakaso ni nini na jinsi iya kuupata. Mwokozi aliomba akisema “Uwatakase kwa ile kweli, neno lako ndiyo kweli. Na Paulo afundishe akisema kuwa wanafunzi lazima watakaswe kwa Roho Mtakatifu” 1Thes. 4:3; Yohana 17:17; Warumi 15:16.TU 227.1

  Kazi ya Roho Mtakatifu ni nini? Yesu aliwafundisha wanafunzi wake akisema “Atakuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote” Yohana 16:13,. Na mtunga Zaburi asema “Sheria yako ndiyo kweli” kwa kuwa sheria ya Mungu ni takatifu, na ya haki na njema, tabia inayofanywa kwa kuitii sheria ya Mungu lazima itakuwa takatifu. Kristo ndiye kielelezo cha tabia takatifu. Naye alisema “Nimeshika amri za Baba yangu” “Kila mara nafanya mapenzi yake” Yohana 15:10; 8:29. Wafuasi wake lazima wafanane naye - kwa neema ya Mungu waumbe tabia inayoambatana na kanuni za utakatifu wa sheria yake. Huu ndio utakaso wa Biblia.TU 227.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents