Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mambo ya Wote Yamekatwa

  Rehema inafungwa muda mfupi kabla ya kuonekana kwa Kristo, akirudi duniani, katika mawingu ya mbinguni. Kristo akitazamia wakati huo, anatangaza akisema “Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo” Ufunuo 22:11-12.TU 238.2

  Watu watakuwa wakipanda na kujenga, wakila na kunywa, wote bila kuwa na habari kwamba tangazo la mwisho limekwisha kutolewa katika patakatifu huko mbinguni.TU 238.3

  Wakati ule kabla ya gharika, baada ya Nuhu kuingia safinani, Mungu alimfungia mlango akiwa ndani, na waliendelea na anasa zao, hali wakidhihaki maneno ya Nuhu. Mwokozi alisema, “Ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake mwana wa Adamu. Kimya, kimya bila kujua, kama mwizi ajavyo usiku, ndivyo itakavyokuwa saa ya kuamuliwa mambo ya mwanadamu.” “Kesheni basi, asije akawajia na kuwakuta mnalala” Mathayo 24:39; Marko 13:35-36.TU 238.4

  Hatari itawakumba wale waliochoka kukesha, na kugeukia mambo ya ulimwengu. Wakati wenye biashara wakiwa katika kufukuzana na uchumi, wakati wapenda anasa wanajishughulisha na anasa, wakati warembo wanaendelea kujipamba, inawezekana katika saa hiyo ndipo tangazo la Mwamuzi wa dunia yote, litasema “Umepimwa kwa mizani ukaonekana umepungua” Daniel 5:27.TU 238.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents