Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  30/Shetani na Mwanadamu Vitani

  “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino”. Mwanzo 3:15. Uadui huu sio wa kawaida. Mtu alipoasi amri ya Mungu hali yake ya asili iligeuka kuwa uovu, ikipatana na hali ya shetani. Malaika waovu pamoja na wanadamu wakapatana. Kama Mungu asingeingilia kati, shetani na wanadamu wangalishirikiana kushindana na mbingu, na kwa njia hiyo watu wote wangejiunga pamoja kuwa wapinzani wa Mungu.TU 246.1

  Shetani aliposikia kuwa kutakuwako uadui kati yake na mwanamke, na kati ya mzao wake na mzao wa mwanamke, alifahamu kuwa kwa vyo vyote mtu atawezeshwa kuwa mpinzani wake.TU 246.2

  Kristo aliuweka uadui katika mwanadamu kumpinga Shetani. Bila kuwa na uwezo huu wa neema uliowekwa kwa mwanadamu, daima angalikuwa mtumishi wa kutenda mapenzi ya shetani. Lakini kanuni mpya rohoni mwa mtu ilianzisha mashindano. Uwezo ambao Kristo alimpa mtu humwezesha kupingana na utawala wa shetani. Kuichukia dhambi badala ya kuipenda huonyesha kanuni ya mbinguni.TU 246.3

  Uhasama baina ya Kristo na shetani ulionekana dhahiri wakati wa kuja kwa Kristo mara ya kwanza, jinsi ulimwengu ulivyompokea. Usafi na utakatifu wa Kristo uliamsha chuki kubwa kati yake na watu wasiomcha Mungu. Hali yake ya kujikana nafsi ilikuwa shutuma kwa mwenye majivuno, mwenye tamaa. Shetani pamoja na malaika waovu waliungana na watu wafedhuli kumpinga mwenye ukweli halisi. Hali ile ile ya uhasama ilionekana kwa wafuasi wa Kristo pia, wakipingana na maovu. Mtu yeyote anayepinga majaribu ya shetani huamsha chuki yake na kumletea mashambulio. Kristo na Shetani hawawezi kupatana. “Wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa” 2Tim. 3:12.TU 246.4

  Wajumbe wa Setani hutafuta kuwadanganya wafuasi wa Kristo, ili kuwaondoa katika njia nyofu ya kuafikiana na Kristo, ili kuwaondoa katika njia nyofu ya kuafikiana na Kristo. Huyapotosha maandiko ili kutimiza makusudi yao maovu. Roho ile iliyomwua Kristo, ndiyo hiyo inayowaamsha waovu kuwaangamiza wafuasi wa Kristo. Haya yote ni kivuli cha lile tangazo la kwanza la unabii kwamba, “Nitauweka uadui kati yako na mwanamke, na kati ya mzao wako na mzao wake”TU 246.5

  Kwa nini shetani hakutani na upinzani mzito? Ni kwa kuwa askari wa Kristo wanashikamana na Kristo kidogo tu. Dhambi haiwachukizi kiasi kikubwa kama ilivyo mchukiza Bwana wao.TU 246.6

  Hawakutani nayo wakiwa na nia kamili ya kuipinga. Wamepofushwa na mkuu wa giza. Watu wengi hawajui kuwa adui yao ni jemadari hodari wa vita, akipingana na Kristo. Hata wachungaji, wahubiri wa Injili hupita tu bila kujali kuwa adui yao halali daima. Hujifanya kana kwamba hawajali kuwako kwake shetani.TU 247.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents