Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Biblia Nzima ni Kiongozi

  Wakati Biblia inaposomwa bila maombi, bila kuwa na nia ya kujifunza, ukweli wake utapotoshwa na kudhanikuwa Biblia inasema hivi, kumbe siyo maana yake. Biblia nzima lazima isomeke kikamilifu bila kuhafifisha sehemu yo yote.TU 254.4

  Mungu alitoa neno la unabii lililo imara, malaika na hata Kristo mwenyewe alikuja kumjulisha Danieli na Yohana mambo yatakayokuwa upesi sana “Ufunuo 1:1 mambo muhimu yahusu- yo wokovu wetu hayakufunuliwa kwa njia ya kutatanisha watu, kiasi cha kupoteza wengine, bali yako wazi kwa mtu anayeutafuta ukweli. Neno la Mungu liko wazi kwa mtu anayeutafuta ukweli. Neno la Mungu liko wazi kwa mtu yeyote anayelisoma kwa roho ya maombi na kujifunza.TU 254.5

  Kule kuwa wafadhili kumewapofusha wengi wasigundue hila za adui wao. Amefaulu kuwapotoshea maana ya Biblia halisi na kuweka badala yake maelezo ya watu. Sheria ya Mungu imetupiliwa mbali, na makanisa yamo katika utumwa wa dhambi, wakati yakidhani kuwa yako huru.TU 255.1

  Mungu amewajalia watu wawe na nuru nyingi ya elimu ya sayansi. Walakini hata wataalamu maarufu wa elimu kama hawaongozwi na Biblia hupotea katika majaribio yao ya uhusianisho baina ya sayansi na Biblia kama inavyofunua elimu halisi.TU 255.2

  Elimu ya kibinadamu ina sehemu tu na sehemu nyngine siyo kamili. Kwa hiyo wengi hawawezi kuhusianisha sayansi na Neno la Mungu. Hujiendea tu na kujidhania kuwa wenye elimu, wasilitambue Neno la Mungu lielezavyo sayansi halisi. 1Tim. 6:20. Kwa kuwa wanashindwa kueleza Mwumbaji na kazi zake katika vita vya asili, na sheria za asili, habari zinazoelezwa katika Biblia huziona kuwa si yakini, na hafifu. Watu wasiotumaini habari za Agano la kale na Agano Jipya, mara nyingi huendelea kiasi cha kutoamini kuwa Mungu yuko. Basi kinachowabakia ni kutangatanga tu, kama meli isiyokuwa na nanga. Huendelea kuishi katika ukafiri, Ni makusudi ya Shetani kuwashikilia watu katika giza la kubahatisha bahatisha, na kujaribu kugundua mambo ambayo Mungu hakuyadhihirisha. Shetani au Lusifa hakuridhika kwa sababu Mungu hakumfunulia siri zake, na makusudi yake, na sasa anawatia watu nia ya namna ile ile, hata wasijali amri za Mungu.TU 255.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents