Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwito wa Shetani Wenye Akili

  Kwa kuwa wataalamu na wenye akili, Shetani huwaingilia kwa njia ya kuwaletea mizuka ya kiroho kwa njia ya akili sana, yaani sura za rafiki na jamaa zao waliokufa, kana kwamba wanaweza kuongea. Hupendelea kuwaza mawazo ya ajabu ya kusisimua na ya utaalamu, yaliyojaa mambo ya upendo na fadhila tele. Huwafanya watu kupendelea mambo ya jinsi hiyo, na kupuuzia mambo ya milele ya Mungu.TU 270.3

  Shetani huwadanganya watu sasa kama vile alivyomdanganya Hawa katika bustani ya Edeni, kwa njia ya kuwafanya wawe na hamu ya kujitukuza. Huwaambia “Mtakuwa kama miungu”, “mkijua mema na mabaya” Mwanzo 3:5. Wenye hali ya mizimu hufundisha kuwa mtu ni kumbe chenye maendeleo …… ambayo huchunguza mambo ya Mungu. Tena, husema, maamuzi yote ni sawa kutokana na ubinafsi. Husema, “Mtawala”. Mwingine husema, “Ye yote wa kweli aliye mkamilifu ni Kristo”TU 270.4

  Hivyo shetani amejiweka na kumweka mtu wa dhambi kama mtaalamu na mtawala wa haki. Haya ni maendeleo, siyo kupanda juu, bali ya kudidimia chini. Mtu hawezi kupanda zaidi ya kipeo chake cha uzuri na wema. Kama kujitukuza nafsi ndilo kusudi la shabaha yake kuu, hataweza kamwe kufika popote. Neema ya Mungu ndiyo pekee yake iwezayo kumkweza mtu. Kama mtu akiachwa ajiendeshe mwenyewe, ataanguka tu.TU 270.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents