Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Vijana Walifundishwa Kuwa Wahubiri

  Wakristo wa Vaudois walijisikia kuwa na wajibu wa kuangaza nuru yao kusiko na nuru. Kwa uwezo wa neno lake Mungu walitafuta kuvunjilia mbali utumwa ulioletwa na Rumi. Wachungaji wa Vausois walifanya kazi nje ya nchi yao muda wa miaka mitatu, kabla ya kurudi nyumbani kufanya kazi huko. Kufanya kazi nje kuliwasaidia kuwa wahudumu bora wafaao kukabili hali zote. Vijana hawakuona kuwa watu wa fahari, au matajiri, bali waliowaona kuwa watu wa kufanya kazi ngumu, wakikabili hatari kwa ujasiri, na mara nyingine kupoteza maisha yao. Wahubiri hawa walikwenda wawili wawili sawa kama wale waliotumwa na Yesu.TU 25.3

  Kazi hiyo ya kutangaza ukweli wa neno la Mungu iliwahatarisha kabisa, kuwafanya wapingwe na Rumi. Kila mchungaji alijua kazi fulani ya ufundi, hivyo kila mchungaji alifanya kazi ya kuhubiri, huku akifanya kuwa ni fundi wa aina fulani au mfanya biashara. Walichukua nyuzi za hariri, lulu, na vitu vingine, kana kwamba ni wafanya biashara, na kumbe ni wahubiri. Walichukua Biblia au sehemu ya Biblia na kuzificha sana zisionekane, na kwa hekima wakaingiza mafundisho ya Biblia kwa watu kwa njia ya siri. Ilipobidi wakaacha maandiko matakatifu kwa watu waliotaka.TU 25.4

  Wahubiri hawa walisafiri katika miji mingi, wakienda kwa miguu na bila viatu, wakiwa na mavazi hafifu. Katika njia zao walimopita makanisa yalijitokeza na damu ya wafia dini ilikuwa mashahidi wa ukweli. Neno la Mungu lilipokelewa kimya kimya katika mioyo ya watu na katika nyumba za watu.TU 26.1

  Waldenses waliamini kuwa mwisho wa ulimwengu hauko mbali sana. Walivyokuwa wakisoma Biblia, waliona kuwa wana wajibu wa kuwaonya watu wengine. Walifarijika sana na kujiona kuwa na amani kuu kwa ajili ya kumwamini Yesu Kristo. Nuru ya Injili iliyowamulikia, waliona haja ya kuwamulikia waliokuwa gizani katika vifungo vya mapapa.TU 26.2

  Watu wengi walifundishwa na mapapa kuwa matendo yao mema yanatosha kuwaokoa. Kwa hiyo daima walijitumaini. Walijitesa kwa kila hali katika mchafuko wa dhamira zao za dhambi, bila kuona furaha yoyote. Watu maelfu waliishi katika majumba ya watawa, walifunga mara kwa mara, na kujitesa, kukesha usiku kucha, kusujudu, na kujigaragaza katika unyevu, kukalia mawe yenye majimaji kwenda safari ndefu na kadhalika. Walirudia mambo hayo mara kwa mara, bila tumaini lolote mpaka dhamira zao zikafilisika, na mwisho wakaingia makaburini bila chembe ya faraja.TU 26.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents