Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Tufani yakaribia

  Kwa kadiri tufani ikaribiavyo, watu waliojidai kuwa waumini katika ujumbe wa malaika wa tatu, lakini hawakutakaswa kwa ile kweli, watauacha uamini wao na kujiunga na upande wa upinzani. Kule kujiunga na ulimwengu wanafahamu mambo ya kanisa vizuri, ingawa si kamili. Watu ambao zamani walikuwa wakilitumikia kanisa vizuri, sasa wanajiunga na upande wa wengi kukwaza wengine na kuwapoteza. Wamekuwa maadui wakali wa wale wa zamani walikuwa wenzao. Waasi hawa ambao sasa wamekuwa wajumbe wa shetani kuvuruga kazi ya Mungu, na kuwainukia watunza sabato, wataomba msaada wa serikali ili kuwaudhi.TU 296.5

  Watumishi wa Bwana wametoa maonyo kwa ukamilifu, kwa kuongozwa na Roho Mtaktifu. Hawakuzuilika kwa kutafuta faida zao, wala kutafuta heshima na vyeo vya duniani. Kazi hiyo ilikuwa kubwa zaidi ya uwezo wao, lakini hawakuiacha. Wakijisikia katika hali ya unyonge na kutoweza kwao, walimkimbilia mweza yote, ili awasaidie.TU 297.1

  Katika vipindi mbalimbali vya historia ya dunia kazi ya Mungu imeonyesha maendeleo makubwa, kufuatana na hali ya watu kwa vipindi hivyo. Kila kipindi ukweli ulipenya katikati ya upinzani. Wajumbe wa Bwana hutimiza wajibu wao, na kumwachia mwenyewe matokeo, yaani Mungu.TU 297.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents