Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Wakati wa Taabu ya Yakobo

  Kwa vile Sabato itakuwa ndilo jambo hasa la kushindania katika ulimwengu wa Kikristo, itaamuliwa kuwa watu wachache wanaosimama peke yao kinyume cha kanisa na serikali, ambao huabudu siku ya jumamosi badala ya jumapili, hawawezi kuvumiliwa zaidi. Ni bora watu wachache washughulikiwe kikamilifu kuliko taifa zima kuingia katika machafuko. Mambo yale yale yaliyoletwa pia kwa Kristo. Kayafa alisema, “Hamfikirii ya kuwa yafaa mtu mmoja afe, kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima” Yohana 11:50. Jambo hili hili litaletwa tena ili kuwapinga washika sabato ya amri ya nne. Itasemwa kwamba, kama hawasikii na kuacha ibada ya jumamosi baada ya muda fulani, afadhali wauawe. Warumi katika ulimwengu wa zamani pamoja na kanisa lililoasi walitumia jambo hili, Waprotestanti waliasi kutoka ulimwengu mpya watafuata njia ile ile. Ndipo watu wa Mungu watakuwa na wakati mbaya, kama ilivyoandikwa kwamba “wakati wa taabu ya Yakobo” Yakobo wakati aliposhindana katika maombi ili aokolewe mikononi mwa Esau, husimama kuwakilisha maisha ya watu wa Mungu wakati wa taabu.TU 300.1

  Yakobo alikimbia kutoka kwao, kwa sababu ya udanganyifu aliofanya ili apate mibaraka ya baba yake iliyokusudiwa kwa Esau. Alikimbia bila silaha yoyote, ili apate kujiponya. Baada ya kukaa katika hali ya ukimbizi miaka mingi, alianza safari kurudi kwao. Alipofika mipakani, alitishwa na habari kwamba Esau alikuwa akimjia, bila shaka kulipiza kisasi. Tumaini la Yakobo lilikuwa kwa Mungu tu; ngao yake ikiwa maombi yake.TU 300.2

  Akiwa peke yake na Mungu, aliungama dhambi zake kwa unyenyekevu na kujidhili mbele za Mungu. Tatizo kuu katika maisha yake limefika. Aliendelea kuomba gizani, kwa ghafla mkono ukamshika begani mwake. Alidhani kuwa ni adui fulani ataka kumwangamiza. Basi akashikana naye kwa nguvu zake zote, akashindana naye. Wakati wa mapambazuko, yule mgeni akatumia uwezo wa pekee usiokuwa wa kibinadamu. Yakobo akaona kuwa amepooza, na akaanguka chini hana nguvu huku akilia na kuomba akiwa shingoni mwa huyo mgeni wa kimiujiza. Halafu alifahamu kuwa malaika wa agano ndiye aliyekuwa akishindana naye. Alikuwa na majuto kwa ajili ya dhambi yake kwa muda mrefu, na sasa lazima awe na hakika kuwa amesamehewa. Malaika akasema, “niache kwani kunapambazuka” lakini mzee Yakobo akasema, “Sikuachi, usiponibariki” Yakobo akatumaini rehema za Mungu kwa kushika maagano. Kwa njia ya toba na kujitoa kikweli, mtu dhaifu huyu alishinda mheshimiwa wa mbinguni.TU 300.3

  Shetani alikuwa amemshitaki Yakobo mbele za Mungu kwa ajili ya dhambi zake, alikuwa amechochea Esau ili amshambulie. Wakati mzee Yakobo alipokuwa akiomba usiku ule, shetani alijitahidi kumfisha moyo na kumkatisha tamaa, ili kuharibu ushirika wake na Mungu. Alikuwa mashakani kabisa; lakini alitubu kweli kweli na kumshikilia malaika, na kusihi apate kibali mpaka akamshinda. Jinsi shetani alivyomshitaki Yakobo, ndivyo atakavyowashitaki watu wa Mungu, lakini kundi linaloshika amri za Mungu litashindana na ukuu wake. Aona kuwa malaika wa Mungu wanawalinda, na anafahamu kuwa dhambi zao zimesamehewa. Anajua dhambi zile alizowashawishi kutenda, kwa hiyo anadai kuwa Mungu hawezi kuwakubali watu wa jinsi hiyo na waangamize shetani na malaika zake. Akasema kuwa watu hao ni mali yake, ili waangamizwe pamoja.TU 301.1

  Bwana humruhusu awajaribu kabisa. Uaminifu wao kwa Mungu, imani yao, na matumaini yao vyote vitajaribiwa na Shetani kabisa kabisa. Shetani atawaogofya kwa bidii yake yote. Hutumaini kuwa kwa kufanya hivyo atavunja matumaini yao, na kuvunja imani yao kwa Mungu, ili wasalimu amri.TU 301.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents