Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mpaka Mji Mtakatifu

  Watu wote waliokombolewa ambao hesabu yao ni kama mchanga, macho yao wote wanamwangalia Yesu. Kila jicho linautazama utukufu wake ambaye, “Uso wake ulikuwa umeharibika sanaa zaidi ya mtu yeyote, na umbo lake zaidi ya wanadamu” Isaya 52:14. Juu ya vichwa vya washindaji, Yesu anaweka taji za utukufu. Kila mtu ana taji yenye jina lake lile jina jipya (Ufunuo 2:17) na andiko lisemalo, “Utakatifu kwa Bwana”. Kila mtu akapewa tuzo ya ushindi, na kinanda au kinubi cha kuimbia, chenye kung'aa sana. Halafu malaika, mwimbaji anapopiga wimbo, kila mtu anashika kinubi chake akiimba kwa ufundi wa ajabu. Kila sauti ikainuliwa kwa sifa za shukrani ikisema, “Kwake yeye atupendaye na kutuoosha dhambi zetu katika damu yake, na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una yeye hata milele na milele” Ufu. 1:5-6.TU 313.5

  Mbele ya jeshi la waliokombolewa uko mji mtakatifu Yesu afungua malango, na mataifa ambao wametunza sheria yake wanaingia ndani. Kisha sauti yake inasikika ikisema, “Njooni mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu” Mathayo 25:34. Kristo anawapeleka watu walionunuliwa kwa damu yake mbele ya Baba yake na kusema “Mimi niko hapa pamoja na watoto ulionipa” “Wale ulionipa, nimewatunza”. Waebrania 2:13; Yohana 17:12. Wakati huo Baba awatazamapo kundi hili la waliokombolewa, naona sura yake mwenyewe ndani yao. Alama ya dhambi imeondolewa, na sasa ubinadamu na Uungu umeungana.TU 314.1

  Furaha ya Mwokozi inazidi anapoona kundi lililokombolewa kutokana na mateso yake. Na wateule hawa watashiriki katika furaha yake. Wanawaona wale waliowahudumia kwa njia ya maombi yao, kazi yao, na sadaka zao. Furaha yao itazidi wanavyoona jinsi muungano wa kazi ulivyo, yaani huyu akamleta yule na yule akamleta wingine kadhalika.TU 314.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents