Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Adamu Wawili Wakutana

  Waliokombolewa walipokaribishwa katika mji wa Mungu, kulikuwa na shangwe kuu, Adamu wawili karibu wakutana. Mwana wa Mungu atampokea baba wa taifa la kibinadamu, ambaye alimwumba, akamtenda dhambi ambazo zilisababisha kusulubishwa kwa Mwokozi, na kupata alama katika mwili wake. Adamu anapoona alama za misumari katika mikono yake, anajitupa chini ya miguu ya Kristo. Mwokozi anamwinua na kumwambia atazame tena bustani ya Edeni, ambayo alifukuzwa kwa siku nyingi.TU 314.3

  Maisha ya Adamu yamekuwa ya huzuni nyingi. Kila mara alipoona majani yakinyauka na alipouona mnyama wa sadaka, ili kumpatanisha na Mungu yote hayo yalimkumbusha ubaya wa dhambi. Aliona uchungu wa ajabu, mambo hayo yote yalipotupwa kwake, kwamba ni yeye aliyesababisha, alijuta kabisa. Akafa katika tumaini. Na sasa kwa kuwa alisamehewa, amerudishiwa hali yake ya kwanza.TU 315.1

  Akijaa furaha tele, aliuona mti wa uzima uliokuwa chakula chake. Akaona miche na miti ambayo yeye alikuwa akiishughulikia kwa mikono yake. Akaona maua mazuri. Kweli Edeni imerudishwa!TU 315.2

  Mwokozi anamwongoza kwenda kwenye mti wa uzima na akaambiwa ale matunda yake. Adamu aliona maelfu ya ukoo wake ambao wamekombolewa. Ndipo akaitupa taji yake miguuni mwa Mwokozi, akamsujudia. Akashika kinubi chake na kuimba kwa shangwe kuu; “Anayestahili, anayestahili ni Mwana Kondoo peke aliyechinjwa”. Ufu. 5:12. Ndipo ukoo wote wa Adamu wakazitupa taji zao miguuni pa Mwokozi wakamwabudu. Wakati Adamu alipoasi malaika waliomboleza, lakini Kristo alipofungua makaburi wakatoka wenye haki huku ilikuwa shangwe kuu. Wakaona kazi ya ukombozi ilivyotimizwa. Ndipo wakaungana na waliokombolewa katika nyimbo za kusifu.TU 315.3

  Juu ya bahari ya kioo iliyochanganyika na moto, likasimama jeshi la washindaji, walipata ushindi juu ya mnyama na sanamu yake, na chapa ya jina lake, na hesabu ya jina lake. Watu mia moja na arobaini na nne elfu waliokombewa kutoka katika watu. Hao waliimba wimbo mpya, wimbo wa Musa na Mwana Kondoo. Ufunuo 15:2-3. Hakuna wengine, ila ni wale mia na arobaini na nne elfu peke yao, ndio waliweza kuimba wimbo huo maana ni wimbo unaohusu mambo yaliyowapata, ambayo wengine hawakuyapitia. “Hawa ndio wamfuatao mwana Kondoo kila mahali aendako” hawa wamebadilishwa kati ya watu hai, ndio malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana Kondoo. Ufunuo 14:4-5.TU 315.4

  Wamepitia wakati wa taabu kuu ambayo ilikuwa haijatokea wamevumilia dhiki ya taabu ya Yakobo; walisimama peke yao bila mtetezi wakati wa mapigo saba ya Mungu. “Wamefua mavazi yao na kuyafanya meupe katika damu ya mwana Kondoo. Katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa”. “Hawataona njaa kamwe, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote.TU 315.5

  Kwa maana huyo mwana Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza katika chemichemi ya maji ya uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao”. Ufunuo 7:14; 14:5; 7:16-17.TU 316.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents