Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shambulio la Mwisho Juu ya Mungu

  Shetani alishauriana na watu hawa hodari. Wakasema kuwa jeshi lililomo mjini ni dogo, ukilinganisha na lao. Kwa hiyo watalishinda tu. Basi mafundi wanaanza kuunda silaha kwa haraka sana. Majemadari wanapanga majeshi katika vikosi vyao.TU 324.1

  Mwisho amri ikatolewa ili kushambulia. Jeshi kubwa mno likaanza kwenda kusogelea mji wa Mungu. Ni jeshi kubwa mno halijapata kutokea vizazi vyote, halihesabiki. Anatangulia shetani na wafalme na majemadari wanakuja nyuma. Wakasikia katika dunia iliyobomoka bomoka wakiuelekea mji wa Mungu. Yesu akaagiza milango ya mji ifungwe. Na jeshi la shetani lajiweka tayari kuushambuliaTU 324.2

  Sasa Kristo akaonekana machoni mwa adui zake. Mbali kule mjini, mahali panapong'aa kwa dhahabu na kuna kiti cha enzi. Juu ya kiti hicho ameketi mwana wa Mungu na kumzunguka wako waliokombolewa, raia zake. Utukufu wa Baba unamzunguka mwanawe. Utukufu wake unang'aa ukipenya mjini mpaka nchi yote ikazungukwa.TU 324.3

  Karibu na kiti cha enzi wanaketi watu waliokuwa watumishi mashuhuri wa shetani hapo kwanza, ambao walinyakuliwa kama kinga cha moto, na sasa wanamtumikia Kristo kwa uaminifu sana. Baada ya hao wako wale walioishi katika nchi ya maovu, lakini wakaishi maisha safi bila kuambukizwa na maovu hayo. Watu walioshika sheria ya Mungu wakati watu wengine walipoasi. Na watu mamilioni waliouawa kwa ajili ya Yesu, watu wa vizazi vyote. Halafu ndipo linakuja “jeshi kubwa, ambalo hakuna mtu awezaye kuwahesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha …. Wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao” Matawi ya mitende ni alama ya ushindi. Mavazi meupe ni alama ya haki ya Kristo, ambayo ni yao sasa.TU 324.4

  Katika kundi hilo lote, hakuna hata mtu anayedai kuwa amepata mambo hayo kwa haki yake na wema wake mwenyewe. Hakuna kitu kisemwacho kuhusu dhiki iliyopatikana duniani. Neno kuu lao ni, “Wokovu una Mungu wetu na mwana kondoo”TU 325.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents