Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mungu amtumia Frederick Saxony

  Jicho la Mungu lisilosinzia lilikuwa likiangalia mienendo ya Luther. Mungu alimwandaa Frederick wa Saxony mtu mwenye moyo safi moyo wa kweli ili amtunze Luther. Katika safari ya kutoka Worms kurudi nyumbani, Luther alitengana na wenzake. Alichukuliwa kwa njia ya msituni kwenda katika gereza la Wartburg, ambako alifungiwa ili kumficha. Maficho yake yalikuwa ya siri hata Frederick mwenyewe hakufahamu. Kwa kuwa ilikuwa siri ya ulinzi Frederick alikaa bila wasiwasi bora tu yu salama. Majira ya kiangazi na masika yakapita, na Luther aliendela kukaa gerezani. Alexander, mfuasi wa Luther alifurahi sana. Nuru ya injili ilionekana kwamba imezimika. Lakini nuru ya Luther iling'aa kwa mng'ao mkubwa.TU 77.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents