Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Pambano Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uvumilivu Wa Mungu

  Mungu alikawiza hukumu yake juu yao kwa muda wa miaka karibuni arobaini. Kulikuwa na Wayahudi wengi ambao hawakuelewa kazi ya Kristo. Tena watoto hawakupata nafasi kama ile ya wazazi wao. Kwa njia ya mahubiri ya mitume nuru ya Injili ingewafikia wote. Wangeona jinsi unabii ulivyotimia, sio kwa kuuliwa kwa Kristo tu, bali kwa kifo na kufufuka kwake pia. Watoto wasingepaswa kupata adhabu kwa ajili ya dhambi za wazazi wao. Lakini walipoikataa nuru iliyowafikia, ndipo wakashiriki dhambi za wazazi wao na kukijaza kikombe cha uovu wao.TU 4.4

  Wayahudi kwa ajili ya ukaidi wao na uasi wao walikataa karama yao ya neema ya mwisho waliyopewa. Ndipo Mungu akawaondolea ulinzi wake. Taifa zima likaachwa liongozwe na kiongozi waliyemchagua. Shetani aliwaamshia hali fedhuli kabisa, nyonge na ya udhalimu. Watu walikuwa kama wanyama tu wakitangatanga kama vipofu, wakawa wakatili. Marafiki na watu wa jamaa moja moja walisalitiana tu wao kwa wao. Wazazi waliwaua watoto wao, na watoto wazazi wao. Watawala hawakuweza kujitawala wenyewe, ukali wao ukawafanya kuwa wajeuri sana. Wayahudi walikubali maneno ya ushahidi wa uongo juu ya Kristo hata wakamwua Yule mwenye haki, Mwana wa Mungu, asiye na hatia. Sasa mashitaka yao ya uongo yamefanya maisha yao kuwa ya ovyo. Hofu ya Mungu haikuwa ndani yao tena. Shetani ndiye alikuwa mtawala wao. Viongozi wa upinzani wakaangamizana wao na wapinzani wao bila huruma. Hata mambo matakatifu ya hekaluni hayakuweza kuheshimiwa. Hekalu lilitiwa unajisi kwa maiti zilizokuwa zikitupwa huko ovyo. Hata hivyo matendo ya kinyama ya jinsi hii waliyoyatenda walikuwa wakiona sawa tu na kusema kuwa waliyoyatenda walikuwa wakiona sawa tu na kusema kuwa Yerusalemu hautaharibiwa, maana ni mji wa Mungu! Hata wakati ule Warumi walipozunguka mji wafedhuli hawa walikuwa na tumaini kuwa Mungu angeingilia kati na kuwafukuza Warumi. Lakini Israeli alikuwa ameondolewa ulinzi wake, na sasa yuko wazi bila kinga yoyote.TU 4.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents