“Jihadharini ... na watenda mabaya... Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili” Wafilipi 3:2, 3. Mar 147.1
Wapo wale ambao wanahitaji mguso wa Roho wa Mungu katika mioyo yao. Ndipo watakapokuwa na mzigo kwa ajili ya ujumbe wa wakati huu. Hawatatafuta viwango vya kibinadamu, wala kitu fulani kipya na cha ajabu. Sabato ya amri ya nne ndiyo jaribio la wakati huu. Amri ya Mungu, ambayo imevunjwa na karibu ulimwengu wote, ndiyo ukweli ambao ni kipimo kwa wakati unakuja ambapo wale wote wanaomwabudu Mungu watatambuliwa kwa ishara hii. Watajulikana kuwa ni watumishi wa Mungu kwa ishara hii ya utii wao kwa Mbingu. Lakini vipimo ambavyo vimewekwa na wanadamu vitaondoa mawazo ya watu kutoka kwenye manfundisho makuu na ya muhimu ambayo yanahusu ujumbe wa leo. Mar 147.2
Ni shauku na mpango wa Shetani kuleta miongoni mwetu watu wenye msimamo kupita kiasi katika maoni yao - watu walio na mawazo finyu, ambao ni wakali na wakosoajl’ na wenye kung’ang’ania dhana zao wenyewe za kile ambacho ukweli unamaanisha. Watakuwa ni washurutishaji. na watataka kulazimisha wajibu mgumu, na kukuza sana mambo ambayo sio ya muhimu sana, huku wakipuuzia mambo makuu zaidi ya sheria-hukumu na rehema na upendo wa Mungu. Kupitia utendaji wa watu wachache kutoka miongoni mwao, jumuia nzima ya washika Sabato itatajwa kama watu ambao ni washupavu wa dini. Mar 147.3
Mungu anayo kazi maalum ambayo watu wenye uzoefu wanapaswa kuifanya lmewapasa kuweka ulinzi katika kazi ya Mungu. Lmewapasa kuhakikisha kuwa kazi ya Bwana haikabidhiwi kwa watu ambao wanahisi kuwa ni haki yao kusonga mbele kwa kutegemea maamuzi yao wenyewe, kuhubiri mambo yo yote ambayo yanawapendeza, na kutowajibika kwa mtu ye yote kwa ajili mafundisho au kazi yao. Hebu turuhusu tu roho hiyo ya kujitosheleza itawale miongoni mwetu, na ndipo tutashudia kukosekana kwa ulinganifu katika utendaji wetu, kukosekana kwa umoja wa roho, usalama wa kazi, na ukuaji bora wa kazi ... Kristo aliomba kwamba wafuasi wake wame na umajo kama ambavyo Yeye na Baba ni umoja. Wale ambao wanatamani kuona ombi hili limejibiwa, hawana budi kupinga mwelekeo wo wote wa mgawanyiko, na kujaribu kudumisha roho ya umoja na upendo miongoni mwa ndugu. Mar 147.4