“Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote; na jirani yako kama nafsi yako” Luka 10:27. Mar 146.1
Je, ni mafundisho gani ambayo vijana Wanakutana nayo wakati wanapoingia ulimwenguni ili kukabiliana na mivuto yake ya kutenda dhambi, kama vile - tamaa ya kupata fedha, burudani na kujiendekeza, maonesho, anasa, vitu vya gharama sana, kujipatia vitu kwa hila, udanganyifu, wizi, na uharibifu? Mar 146.2
Umizimu unadai kwamba watu ni nusu miungu ambao hawakuanguka dhambini; kwamba ‘kila mtu atajihukumu mwenyewe’; kwamba “maarifa ya kweli yanawafanya watu wawe juu ya sheria yote”; kwamba “dhambi zote zilizotendwa hazina ubaya”; kwani “jambo lo lote lile ni sahihi” na“Mungu hatalihukumu.” Umizimu unaonesha kuwa wanadamu waliokuwa waovu sana, sasa wako mbinguni wakiwa wametukuzwa mno. Na hivyo Umizimu unawatangazia watu wote kuwa “bila kujali kile unachofanya; ishi tu kama upendavyo, mbinguni ni makao yako.” Kwa njia hii maelfu wanaongozwa kuamini kuwa tamaa ni sheria kuu kuliko zote, kwamba kukiuka sheria ni uhuru, na kwamba mwanadamu anawajibika kwake binafsi. Mar 146.3
Je, ulinzi wa maadili uko wapi ikiwa mafundisho kama haya yanatolewa tangu utotoni, wakati nguvu ya msukumo ni kubwa sana na hitaji la kujizuia na usafi likiwa la haraka zaidi? Je, ni kitu gani ambacho kitauzuia ulimwengu usiwe Sodoma ya pili? Mar 146.4
Wakati uo huo utawala huria unatafuta kufutilia mbali sheria zote, za Mungu na za wanadamu. Kukusanya utajiri na madaraka yote sehemu moja, mchanganyiko mkubwa kwa ajili ya kuwatajirisha wachache kwa hasara ya wengi; muungano wa tabaka la watu maskini kwa ajili ya kutetea maslahi na madai yao; ... kuenea ulimwenguni pote kwa mafundisho yale yale yaliyopelekea Mapinduzi ya Ufaransa-vyote vinaelekea kuuhusisha ulimwengu wote katika mapambano ambayo yaliitikisa Ufaransa. Mar 146.5
Mivuto kama hii ndiyo ambayo vijana watakutana nayo siku hizi. Ili kusimama imara katikati ya mageuzi ya jinsi hiyo, hawana budi kujenga misingi ya tabia. Katika kila kizazi na kila nchi, mwelekeo na msingi wa kweli kwa ajili ya ujenzi wa tabia umekuwa ni uleule. Sheria takatifu isemayo, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote ... na jirani yako kama nafsi yako” (Luka 10:27), ambayo ndiyo kanuni kuu iIiyodhihirishwa katika tabia na maisha ya Mwokozi wetu, ndiyo msingi pekee ambao ni salama na mwongozo pekee ulio wa hakika. Mar 146.6