“Sitaweka mbele ya macho yangu neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, haitaambatana nami. Moyo wa ukaidi litaondoka kwangu, lililo ovu sitalijua” Zaburi 137:3, 4. Mar 145.1
Unayo sababu ya kuwa na wasiwasi mkubwa kwa ajili ya watoto wako ambao wanakabiliwa na majaribu katika kila hatua wanayopiga. Haiwezekani kwao kuepuka kabisa kuonana na wenzao ambao ni waovu... Wataona maono, watasikia sauti, na kuwekwa chini ya mvuto wenye kupotosha na ambao, kama hawalindwi vizuri, mvuto huo, bila kutambuliwa lakini kwa uhakika, utaichafua mioyo yao na kuharibu tabia zao. Mar 145.2
Baadhi ya kina baba na kina mama ni wazembe na wasiojali, na wanadhani kuwa hakuna tofauti yoyote kwa watoto wao kusoma katika shule za Kanisa au za Serikali. Wanasema kuwa, “Tumo ulimwenguni na hatuwezi kujitenga nao.” Lakini, enyi wazazi, tunaweza kupata njia nzuri ya kujitenga na ulimwengu ikiwa tutachagua kufanya hivyo. Tunaweza kujizuia kuona maovu mengi ambayo yanazidi kuongezeka katika siku hizi za mwisho. . . Mar 145.3
Kwa akili zenye nguvu za watoto na vijana, matukio yanayoelezwa katika mafunuo ya kufikirika tu juu ya siku za usoni, kwao ni mambo halisi. Kadiri mapinduzi yanavyotabiriwa na kueleza namna zote za mwendelezo wa matukio ambayo yanaondoa vizuizi vya sheria na kujizuia, wengi wanapokea roho ya maonesho hayo. Na kwa hivyo, kama ikiwezekana, wataongozwa kutenda uhalifu mbaya zaidi kuliko ule ambao limeelezwa na waandishi wa vitabu hivyo. Na kwa kupitia mivuto ya jinsi hiyo jamii inapotoshwa. Mbegu za uasi huwa zinapandwa kwa watu wengi. Na hatupaswi kushangazwa kuwa matokeo yake ni ongezeko la uhalifu. . . Mar 145.4
Kwa ujasiri, sema kwamba, “Sitatumia muda ulio wa thamani kwa kusoma yale ambayo hayana faida kwangu, na ambayo yananifanya nisifae kuwahudumia wengine. Nitautoa muda wangu na mawazo yangu ili niweze kustahili kwa ajili ya kazi ya Mungu. Sitaangalia mambo maovu na ambayo hayana maana. Masikio yangu ni mali ya Bwana, nami sitasikiliza udanganyifu uliofichika wa yule adui. Sauti yangu haitatawaliwa na nia ambayo haiko chini ya mvuto wa Roho wa Mungu. Mwili wangu ni hekalu la Roho Mtakatifu, na uwezo wangu wote utatumika kwa ajili ya kazi iliyo njema. Mar 145.5