“Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi ..Ufunuo 6:12. Mar 149.1
Unabii hauelezei tu kusudi na namna Kristo atakavyokuja, bali pia unaonesha ishara ambazo kupitia hizo, watu watatambua kuwa kuja kwake kumekaribia ... Na hivyo mwandishi wa kitabu cha Ufunuo anaelezea ishara ya kwanza kati ya zile zitakazotangulia marejeo ya Kristo: “Nami nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, palikuwa na tetemeko kuu la nchi, jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu.” Mar 149.2
Ishara hizi zilishuhudiwa kabla ya kuanza kwa karne ya kumi na tisa. Katika utimilizo wa unabii huu, mnamo mwaka 1755, kulitokea tetemeko kubwa sana la ardhi ambalo halikuwahi kushuhudiwa. Japokuwa linajulikana zaidi kama tetemeko la Lisbon, lakini lilienea katika sehemu kubwa ya bara la Ulaya, Afrika, na Amerika. Mtikisiko wake ulienea hadi Greenland, Visiwa vya West Indies, Madeira, Norway na Sweden, Uingereza na Ireland. Lilienea na kusikika kwenye eneo la maili mia nne za mraba. Mar 149.3
Mtikisiko uliotokea Afrika ulikuwa ni mkubwa karibu sawa tu na ule ambao (ilitokea Ulaya. Sehemu kubwa ya nchi ya Algeria iliharibiwa: na nje kidogo ya Morocco, kijiji kizima kilichokuwa na watu wapatao elfu nane hadi kumi, kiliangamizwa. Wimbi kubwa sana liligharikisha pwani ya Hispania na Afrika, likimeza miji na kusababisha uharibifu mkubwa. Mar 149.4
Katika nchi za Hispania na Ureno ndiko ambako athari kubwa za mtikisiko huo ziliposhuhudiwa. Katika mji wa Cadiz, mawimbi yalisemekana kufikia kimo cha futi sitini. Milima, “baadhi ya milima mikubwa nchini Ureno ilitikisika kabisa.”. . . - Sir Charles LyelI, Principles of Geology, uk. 495. ‘’Tetemeko hilo lilitokea siku ya Jumapili ambapo makanisa na nyumba za watawa zilikuwa zimefurika watu, na miongoni mwao ni wachache tu ambao walisalimika.” - Encyclopedia Americana, art. “Lisbon,” note (ed. 1831). . . Inakisiwa kuwa watu wapatao elfu tisini walipoteza maisha katika siku ile ya maafa makubwa. Mar 149.5
Kila mara tunasikia juu ya matetemeko ya nchi na vimbunga, uharibifu ambao umetokana na moto na mafuriko, pamoja na uharibifu wa mali na kupotea kwa maisha ya watu! Inavyoonekana, haya majanga ni matokeo ya milipuko isiyoweza kudhibitiwa ya nguvu za asili, ambazo haziwezi kutawaliwa na mwanadamu: lakini katika majanga hayo, kusudi la Mungu linaweza kujulikana. Majanga hay a ni miongoni mwa vitu ambavyo Mungu atavitumia kuwaamsha watu ili waweze kutambua hatari inayowakabili. Mar 149.6