“Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na itishayo.” Yoeli 2:31. Mar 150.1
Katika mazungumzo ya Mwokozi pamoja na wanafunzi wake katika mlima wa Mizeituni, baada ya kuwa ameelezea juu ya kipindi kirefu cha kujaribiwa kwa kanisa, yaani - miaka 1260 ya mateso kutoka kwa mamlaka ya upapa ambapo aliahidi kuwa kipindi hicho kitafupishwa - alitaja pia matukio fulani ambayo yatatangulia kabla ya kuja kwake, na akaweka muda maalum ambapo tukio la kwanza lingeshuhudiwa: “Lakini mara, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake.” Siku au miaka 1260 iliishia mwaka 1798. Karibia robo karne kabla, mateso yalikuwa ni kama yamekoma kabisa. Kufuatana na maneno ya Kristo, baada ya mateso hayo, jua lingetiwa giza. Mei 19, 1780, unabii huu ulitimia. Mar 150.2
“Siku ya tarehe 19 Mei 1780, inasimama kama siku ya ajabu na yenye tukio la aina yake ambalo haliwezi kuelezewa sawasawa, yaani - anga lote la Kaskazini-Mashariki mwa Marekani lilikuwa giza.” — R. M. Devens, Our First Century, uk. 89. Mar 150.3
Saa moja au mbili kabla ya machweo, giza nene la siku hiyo IiIifuatiwa na anga lililokuwa na mawingu kidogo na jua likaonekana, japokuwa lilikuwa bado halionekani vizuri kwa sababu ya ukungu mzito na mweusi. “Baada ya jua kuzama, mawingu yalitanda hadi usawa wa kimo cha mtu na giza liIitanda upesi sana.” “Giza la usiku huo halikuwa la kawaida na lilikuwa linaogopesha sawa na lile la mchana: na licha ya mwezi kuwapo angani, hakuna kitu ambacho kilionekana kwa urahisi isipokuwa kwa msaada wa vitu vya kumulikia ...” - Isaiah Thomas, Massachusetts Spy: or, American Oracle of Liberty, vol. 10, No. 472 (May 25, 1780). Mar 150.4
Maelezo ya tukio hili, kama yalivyotolewa na wale walioshuhudia, ni mwangwi wa maneno ya Bwana ambayo yaliandikwa na nabii Yoeli, miaka elfu mbili na mia tano kabla ya kutimia kwa unabii huo: “Jua litatiwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya BWANA iliyo kuu na itishayo.” Mar 150.5
Kristo aliwataka watu wake waangalie ishara za marejeo yake na wafurahi watakapoona ishara za Mfalme wao ajaye. Mar 150.6