“... Na nyota zitaanguka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika.” Mathayo 24:29. Mar 151.1
Mnamo mwaka 1833, ishara ya mwisho kati ya zile ambazo Mwokozi aliahidi kuwa zitakuwa ni ishara za kuja kwake, ilionekana. Yesu alisema, “Nyota zitaanguka kutoka mbinguni.” Na katika kitabu cha Ufunuo, Yohana anaeleza mambo aliyoyaona akiwa katika maono kuhusu matukio yatakayotangulia siku ya Mungu, “Na nyota zikaanguka juu ya nchi kama vile mtini upukutishavyo mapooza yake, utikiswapo na upepo mwingi.” Unabii huu uIitimia kwa namna ya pekee na ya kuvutia katika tukio la Novemba 13, 1833 la kuanguka kwa vimondo. Hili lilikuwa ni tukio la ajabu IiIilowahi kuandikwa la kuanguka kwa nyota na ambalo lilitokea katika eneo kubwa; “kwa saa kadhaa, anga lote la Marekani halikuwa katika hali ya kawaida! Hakuna tukio lo lote la angani ambalo limewahi kutokea katika nchi hii langu ilipoanza kukaliwa, ambalo liliangaliwa kwa shauku kubwa na tabaka moja la watu katika jamii, au kwa hofu na tahadhari kubwa na tabaka lingine.” “Uzuri na mvuto wake bado vinadumu katika mawazo ya wengi . . . Mvua haikuwahi kunyesha kwa wingi kuliko ambavyo vimondo vilianguka kutoka mbinguni; hali ilikuwa ni ileile mashariki, magharibi, kaskazini, na kusini. Kwa kifupi, anga lote lilionekana kujongea. . . . Kama ilivyoelezwa katika jarida la profesa Silliman, ni kwamba tukio hilo lilishuhudiwa katika bara lote la Amerika ya Kaskazini. . . . Kuanzia saa nane hadi mapambazuko, anga lilijawa na vitu vilivyokuwa vinang’aa na kuvutia sana.” R. M. Devens, American Progress: au The Great Events of the Greatest Century, sura ya 28, paragrafu ya 1 -5. Mar 151.2
Hivyo ndivyo ilivyoonekana ishara ya mwisho ya kuja kwa Yesu ambayo aliwaambia wanafunzi wake kuwa, “Myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu milangoni.” Baada ya ishara hizo, Yohana aliona wakati tukio lililokuwa Unafuata lilipotukia, mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, huku dunia ikitikisika, milima na visiwa vikahamishwa kutoka mahali pake, na waovu waliojaa hofu wakijaribu kuukimbia uso wa Mwana wa Adamu. Mar 151.3
Lakini Kristo hakuweka wazi siku na saa ya kuja kwake . .. Wakati hasa wa kuja kwa Mwana wa Adamu mara ya pili ni siri ya Mungu. Mar 151.4