Go to full page →

Imani Itendayo Kazi, Sura ya 50 Mar 58

Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala. 1 Petro 4:7 Mar 58.1

Je, unaamini ya kwamba mwisho wa mambo yote umekwishafika, ya kwamba matukio ya historia ya dunia hii yanafikia hitimisho kwa kasi? Kama ni hivyo, basi onesha imani yako kwa matendo yako. Mtu anapaswa kuonesha imani yote aliyo nayo. Wapo baadhi ya watu ambao wanadhani ya kwamba wanacho kiwango kizuri cha imani, wakati ambapo kama ipo imani yoyote ndani yao, imeshakufa, kwa sababu haionekani katika matendo. “Vivyo hivyo imani, isipokuwa na matendo, imekufa nafsini mwake.” Ni wachache walio na imani ya kweli itendayo kazi kwa nguvu ya upendo ikitakasa roho. Lakini wale wote wanaoitwa ili kustahili uzima wa milele wanapaswa kuwa na kiwango cha maadili kinachopelekana na uzima huo. “Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.” Hii ndiyo kazi iliyo mbele yenu... Mar 58.2

Sharti nafsi ife, kisha ni lazima uwe hai katika Mungu. “Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.” Usitafute maelekezo ya nafsi. Kiburi, kupenda nafsi, ulafi, tamaa, upenzi wa dunia, chuki, kutokuaminika, wivu, masengenyo, hisia mbaya, zapaswa zote zishindwe na kuachwa milele. Wakati Kristo atakapotokea, hautakuwa wakati kwa ajili ya kurekebisha haya na kisha kutoa mwonekano sahihi wa kimaadili ufaao kwa ajili ya ujio huo. Maandalizi yote haya yanapaswa kufanywa kabla ya kuja kwake. Hili lapaswa kuwa wazo kuu, ambalo tunapaswa kujifunza, na kwa hili kujihoji kwa dhati, “Tufanye nini ili tupate kuokoka?” Je, twapaswa kuwa na mwenendo gani ili tujioneshe kuwa tumekubaliwa na Mungu? Mar 58.3

Unapojaribiwa kunung’unika, kulaumu na kuonesha maudhi, huku ukijeruhi wale walio karibu nawe, na kwa namna hiyo ukijijeruhi roho yako mwenyewe, hebu hoja ya ndani kabisa, ya dhati, yenye shauku itoke katika roho yako, “Je, nitasimama bila ya hatia mbele za kiti cha enzi cha Mungu? Ni wale tu wasio na hatia wakataokuwa pale. Hakuna watakaobadilishwa na kuingia mbinguni wakati mioyo yao imejazwa na taka za dunia. Kila dosari katika maadili inapaswa kurekebishwa kwanza, kila doa liondolewe kwa damu itakasayo ya Kristo, na kila tabia isivopendeka iwe imeshindwa. Mar 58.4