Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani. 1 Timotheo 4:l Mar 59.1
Baada ya kupita kwa ule wakati wa 1844, tulikabiliwa na mafundisho yaliyokithiri ambayo yalikuwa ya kila namna. . . Uzoefu huu utarudiwa. Katika siku za usoni, itikadi za kishirikina Shetani zitaonekana katika mfumo mpya. Makosa yatawasilishwa katika namna ipendezayo na kuonekana kukubalika. Nadharia za uongo, zilizovishwa mavazi ya nuru, zitawasilishwa kwa watu wa Mungu. Kwa namna hiyo, Shetani atajaribu kudanganya yumkini hata walio wateule. Mivuto mikali zaidi itawekwa; na mawazo yatapumbazwa. Mar 59.2
Upotovu wa kila aina, unaofanana na ule uliokuwepo kabla ya gharika, utaletwa ili kuteka mawazo. Kutukuzwa kwa viumbe vya asili na kuvifanya kama Mungu, uhuru mkubwa wa moyo wa mwanadamu, mashauri ya wasiomcha Mungu - haya yote Shetani anayatumia kama mawakala wake ili kufikia miisho fulani maalum. Atatumia nguvu ya mawazo yake kwa akili za kibinadamu ili kukamilisha mipango yake. Wazo la kusikitisha kuliko yote ni lile linalofundisha kwamba chini ya mvuto wake mdanganyifu watu watakuwa na namna ya utauwa, hata bila ya kuwa na muunganiko halisi na Mungu. Kama ilivyokuwa kwa Adamu na Hawa, walipokula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya, wengi hata sasa wanajilisha chembe za makosa haya ya udanganyifu. Mar 59.3
Mawakala wa Shetani wanavisha mafundisho haya mavazi yanayovutia, kama jinsi ambavyo Shetani katika bustani ya Edeni alivyojificha na kuongea na wazazi wetu wa kwanza kupitia kwa Joka. Mawakala hawa wanaingiza taratibu kwenye mawazo ya mwanadamu kile ambacho kwa hakika ni makosa ya kutisha. Mvuto unaopumbaza wa Shetani utawakalia wale wanaoacha neno lililo wazi la Mungu na kugeukia masimulizi yasiyo ya kweli yanayoonekana kupendeza. Mar 59.4
Ni wale ambao wamekuwa na nuru kwa kiasi kikubwa ambao Shetani kwa shauku kubwa zaidi anatafuta kuwatega. Anajua ya kwamba kama akifanikiwa kuwadanganya, watavaa dhambi pamoja na mavazi ya haki chini ya uongozi wake, na kuongoza wengi upotevuni. Mar 59.5
Nasema kwa wote: Iweni macho; kwani Shetani kama malaika wa nuru anatembea katika kila kusanyiko la wafanyakazi Wakristo, na katika kila kanisa, akijaribu kuvuta washiriki upande wake. Ninawajibika kuwapa watu wa Mungu onyo: “Msidanganyike; Mungu hadhihakiwi. Gal. 6:7. Mar 59.6