Mwokozi aligeukia mbali kutoka kwa Mafarisayo, akatafuta watu wengine ambao watasikiliza ujumbe wake wa mbinguni. Akapata wavuvi, watoza ushuru, katika soko, mwanamke wa Samaria, na kwa watu wa kawaida tu, ambao watasikiliza ujumbe wake, kwa watu wa namna hii alipata viriba vyake vya kuwekea divai. Watu hao waliupokea mwanga wake kwa furaha, ambao Mungu aliwatuma wajumbe wake wautangaze. TVV 150.4
Mafundisho ya Kristo yanayofananishwa na divai mpya hayakuwa mafundisho mapya, ila ni yale yaliyofundishwa tangu mwanzo. Lakini kwa Mafarisayo, mafundisho ya Kristo yalikuwa mapya kwa kila hali nayo hayakutambuliwa, wala kukubaliwa. TVV 151.1
“Hakuna mtu anywaye divai kuu kuu, anayetamani divai mpya, maana husema, Divai kuu kuu ni bora.” Ukweli uliotolewa kwa wazee wa zamani na manabii uling’aa kwa uzuri wa neno la Kristo. Lakini waandishi na Mafarisayo hawakuwa na haja ya divai mpya. Hawana haja ya mafundisho ya Kristo, mpaka kwanza mapokeo na kawaida zote za ovyo, viondoke katika mioyo yao. TVV 151.2