Go to full page →

Hatari ya kushikilia mawazo TVV 151

Hali hii ilithibitisha maanguko ya Wayahudi, nayo itathibitisha maanguko katika siku zetu. Watu wengi hukataa nuru itokayo kwa Baba wa nuru zote, kuliko kuyakataa mawazo yao wanayoshikilia. Hushikilia kusema kuwa wameokoka kwa njia fulani na kukamilisha jambo muhimu. Wasipoona njia yoyote, hukanusha wokovu uliomo. TVV 151.3

Dini ya mfano haina upendo. Dini isiyo ya Kristo. Kufunga na kuomba kwa kujipendekeza ni chukizo mbele za Mungu. Matendo yetu wenyewe hayawezi kutuletea wokovu. Kwa watu wasioelewa hali yao ya kiroho jinsi ilivyo, ujumbe huwajia; “Maana wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja na kitu, nawe hujui kuwa u mnyonge, mtu wa kuhurumiwa, kipofu, na uko uchi. Kwa hiyo nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane.” Ufunuo 3:17, 18. Imani na upendo ni dhahabu. Lakini kwa wengi wao dhahabu imefifia, utajiri wake umepotea. Haki ya Kristo ni vazi na chemchemi isiyoguswa. TVV 151.4

“Dhabihu ya Mungu ni roho iliyovunjika, moyo iliyovunjika na kupondeka ee, Mungu hutaidharua.” Zaburi 51:17. Ubinafsi unapoachwa, Bwana humfanya mtu kuwa kiumbe kipya. Kiriba kipya chaweza kuhifadhi divai mpya. Upendo wa Kristo unaweza kumpa mwamini maisha mapya. Ndani yake tabia ya Kristo itaonekana. TVV 151.5