Nikodemo, mtu mwenye elimu kubwa, mheshimiwa sana, ambaye ni mbunge wa laifa la Kiyahudi, alikuwa ametatanishwa kwa mafundisho ya Yesu. Ingawa ni mtu tajiri, na mwenye elimu kubwa, alikuwa amevutiwa na tabia nyenyekevu ya mtu wa Nazareti. Mafundisho ya Mwokozi yalikuwa yamemwingia sana Nikodemo, naye aiitaka kujifunza zaidi mambo hayo. TVV 88.1
Tendo la Kristo la kutakasa hekalu kwa nguvu, lilikuwa limeanzisha chuki kwake toka kwa makuhani na wakuu wa Kiyahudi. Kule kuamuru kwa mtu huyu wa Galilaya, na kufukuza watu hekaluni, kusingaliweza kuachwa hivi hivi, bila kushughulikiwa. Lakini sio wote waliokubaliana kumshughulikia Yesu. Wengine waliogopa kumpinga mtu ambaye anaonekana wazi kuwa anaongozwa na Roho wa Mungu. Walifahamu kuwa mateso wanayopatiwa na watu wa mataifa, yanakuja kwa ajili ya uasi wao na ugumu wao, maana hawayakubali maonyo ya Mungu. Waliogopa kuwa, kufanya njama juu ya Yesu, ni kufuata njia ya uasi kama baba zao walivyofanya. Hayo ndiyo mashauri ya makuhani na wakuu. Na kukubali mambo hayo kutawaletea ajali kubwa zaidi. TVV 88.2
Nikodemo, alikubaliana na watu waliojisikia hivyo. Katika baraza la Sanhedrin, Nikodemo aliwaonya kuwa waangalifu. Alisema kuwa, kama Yesu alikuwa na mamlaka ya Mungu, itakuwa hatari kumkanusha. Makuhani hawakulijali shauri hilo. TVV 88.3
Nikodemo alikuwa amechunguza kwa bidii na kwa hamu kubwa, unabii unaomhusu Masihi. Kadiri alivyochunguza ndivyo aliyozidi kuamini kuwa Yesu ndiye yule atakayekuja, kama unabii unavyosema. Alikuwa amesikitishwa sana na kufuru za watu. Alikuwako wakati Yesu alipowafukuza wenye biashara hekaluni. Aliona Mwokozi akiwaponya wagonjwa; aliona walivyomshangilia kwa shangwe, na kusikiza maneno ya kumtukuza. Hakuwa na shaka kwamba Yesu wa Nazareti in Mwana wa Mungu. Alitamani wakutane na Yesu na kuongea naye. Lakini alisita kukutana naye waziwazi. Maana kama angeonekana na wana baraza wa Sanhedrin ngalijiletea lawama bure na kudhihakiwa. Alikusudia kukutana naye kwa siri. Alipojua kuwa Mwokozi huenda kulala katika mlima wa Mizeituni, alingoja mpaka watu wamelala, ndipo akaenda kumwona Yesu. TVV 88.4
Akiwa mbele ya Yesu, Nikodemo aliona haya, lakini alijitahidi kujikaza, akasema: “Rabi, tunajua ya kuwa wewe ni mwalimu, atokaye kwa Mungu; maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe; isipokuwa Mungu awe pamoja naye.” Maneno yake yalionyesha kuwa anataka mazungumzo. Walakini yalionyesha hali ya kutoamini. Hakumkiri Yesu kuwa ndiye Masihi, ila alisema kuwa ni mwalimu atokaye kwa Mungu. TVV 89.1
Yesu alimwangalia Nikodemo, kama mtu asomaye moyo wake. Alimwona kuwa ni mtafuta ukweli. Yesu alitaka kuimarisha imani yake, alisema: “Amini, amini nakuambia, Mtu asipozaliwa kutoka juu, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.” Yohana 3:3. TVV 89.2
Nikodemo amekuja ili wajadiliane na Yesu, lakini sasa amefunua wazi kanuni za ukweli wote. Alimwambia unachohitaji si kuelewa mambo yalivyo, ila unahitaji kuwa na moyo mpya. Inakupasa upokee hali mpya kutoka juu kwanza, ndipo utafurahia mambo ya mbinguni. Usipokuwa na hali hiyo, haitakuwa na maana yoyote, kujadiliana na mimi kuhusu uwezo wangu na kazi yangu. TVV 89.3
Nikodemo alikuwa amesikia mahubiri ya Yohana Mbatizaji kuhusu kutubu. Walakini mahubiri hayo, ambayo ni ya kufikirisha sana, yalikuwa yameshindwa kumtubisha Nikodemo. Alishikilia hali ya Ufarisayo kamili, na alijivunia matendo yake mema. Alihesabiwa kuwa mtu mtawa sana, hivyo alijisikia kuwa yu salama, mkamilifu wa Mungu. Alishituka kusikia kuwa katika hali hiyo aliyo nayo sasa hawezi kuuona ufalme wa Mungu. TVV 89.4
Namna ya kuzaliwa mara ya pili haikufahamika kwake. Kuongoka rohoni, kulifananishwa na mtoto aliyezaliwa. Kwa hiyo Nikodemo hakuyaelewa maneno ya Kristo. Lakini sawa kama Waisrael wengine, hakuona kuwa anahitaji badiliko lolote. Kwa hiyo alishitushwa kwa maneno ya Mwokozi. Kiburi na majivuno ya Mfarisayo huyu vilitiwa wasiwasi sana, maana anatamani kupata ukweli wote. Nikodemo akiwa na mshangao kwa ajili ya maneno hayo alijibu kwa mzaha, akasema: “Awezaje mtu kuzaliwa akiwa mzee?” Kama watu wengine walivyo, alieleza kuwa kitu cha kiroho kinacholinganishwa na kitu cha asili, maana mambo ya kiroho ni mambo ya kiroho tu, hujulikana kwa hao yenyewe. TVV 89.5
Mwokozi akinyosha mikono yake juu, aliusema ukweli kamili: “Amin, amini nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.” Hapa Nikodemo alijua kuwa Kristo anasema juu ya ubatizo wa maji, na kufanywa upya kwa uwezo wa Roho wa Mungu. Alifahamu kwamba, anasimama mbele ya yule aliyesemwa na Yohana kuwa atakuja nyuma yangu. TVV 90.1