Wakati Yesu alipokuwa akizungumza, nuru ya ukweli ilipenya na kuingia moyoni mwa mkuu huyu. Walakini alikuwa bado kuelewa vizuri maneno ya Mwokozi. Akauliza, huku akishangaa mambo haya yanawezaje kuwa?” Yesu akajibu: “Wewe uliye mwalimu wa Israeli, hujui mambo haya?” Badala ya kuchangamka, Nikodemo angalipaswa kunyenyekea na kujidhili kwa ajili ya ujinga wake wa kutojua mambo. Walakini Yesu alimzungumzia kwa ufasaha sana ili asichukizwe. Lakini Yesu alipomweleza kuwa kazi yake ni kusimamisha ufalme wa kiroho, wala si wa dunia, Nikodemo alitiwa wasiwasi. Yesu alipoona hivyo, aliongeza kusema: “Kama nimekuambia mambo ya dunia, nawe hukuamini, utaaminije nikikuambia mambo ya mbinguni?” Ikiwa hakufahamu kazi ya Yesu duniani, atafahamuje kazi yake mbinguni? TVV 91.2
Wayahudi walifukuzwa na Yesu hekaluni, walikuwa na juhudi ya kujionyesha kuwa ni watakatifu kijuujuu, lakini hawakuwa watakatifu mioyoni. Walikuwa na juhudi kukariri sheria, huku wakiziasi mioyoni mwao. Haja yao kubwa ilikuwa kubadilika katika maisha kama Yesu alivyomwambia Nikodemo, yaani kuzaliwa upya kiroho, kutakasika kutokana na dhambi, na kufanywa upya katika utakatifu. TVV 91.3
Hapakuwa na udhuru kwa Waisraeli kuhusu mabadiliko ya mioyo. Daudi alikuwa ameomba: “Ee Mungu uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.” Ahadi ilitolewa kwa njia ya Ezekieli: “Nitawapa roho mpya, nitawawekea moyo mpya, nitawondolea moyo wa jiwe, nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia ndani yenu Roho yangu, ili mwenende katika amri zangu.” Zaburi 51:10; Ezekieli 36:26, 27. Nikodemo sasa alianza kufahamu maana ya fungu hili. Akaona kuwa kung’ang’ania kushika na kukariri kariri sheria hakutaweza kamwe kumpeleka mtu mbinguni. TVV 91.4
Nikodemo alivutwa kwa Kristo sasa. Mwokozi alipomweleza habari ya kuzaliwa upya, alitamani hali hiyo ionekane kwake mwenyewe. Itafanyikaje? Yesu akasema: “Kama Musa alivyomwinua nyoka wa shaba jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuli wa, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” TVV 92.1
Mfano wa kuinuliwa kwa nyoka kulimfanya Nikodemo aelewe kazi ya Mwokozi. Wakati Waisraeli walipokuwa wakifa kwa kuumwa na majoka, Mungu alimwambia Musa atengeneze nyoka wa shaba, na kumwinua katikati ya mkutano. Wote watakaomwangalia wangeliishi. Nyoka wa shaba alikuwa mfano wa Kristo. Kama mfano ulivyofanywa wa nyoka aharibuye, aliinuliwa kwa ukombozi wao. Vivyo hivyo aliyetwaa hali ya binadamu mwenye dhambi, ndiye atakuwa Mwokozi wao. Warumi 8:3. Mungu alitamani kuwaongoza Waisraeli wamwone Mwokozi. Wamwone kwa kuponywa majeraha yao au kwa kusamehewa dhambi zao. Wasingeweza kufanya lolote kwa nguvu zao, ila wamwamini Yesu, ambaye ni kipawa cha Mungu, Iliwapasa kumwangalia na kuishi. TVV 92.2
Wale walioumwa na nyoka, wangelidai wafahamu kwa njia ya kitaalam. Lakini hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu kupona kwao. Waliokataa kuangalia waliangamia. Nikodemo alilipokea fundisho hilo akalikubali. Alichunguza maandiko ili apate uzima kwa kuamini na kujitoa zaidi. Roho Mtakatifu akamwongoza, naye akakubaliana na uongozi huo. TVV 92.3
Leo watu maelfu wanahitaji kujifunza fundisho lile la kuinuliwa kwa nyoka, alilojifunza Nikodemo. “Hakuna jina jingine chini ya mbingu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” Matendo 4:12. Tunapokea neema ya Mungu kwa imani, lakini imani siyo wokovu wetu. Haileti chochote. Ni mkono tu unaoweza kumshika Kristo, ambaye ndiye dawa ya dhambi. Hatuwezi hata kutubu bila msaada wa Roho wa Mungu. Maandiko husema juu ya Kristo Mtu huyu Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisrael toba na msamaha wa dhambi.” Matendo 5:31. Toba hutoka kwa Kristo, kama vile msamaha wa dhambi. TVV 92.4
Sisi basi tutaokolewaje? “Tazama Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yohana 1:29. Nuru inayong’aa kutoka msalabani huufunua upendo wa Mungu. Upendo wake hutuvuta kwake. Tusipokaidi upendo huu tutaongozwa mpaka chini ya msalaba kwa kutubu dhambi zile zilizomsulubisha Mwokozi. Halafu Roho wa Mungu huleta uzima mpya kwa imani. Ndipo mawazo, na hamu ya mtu humtii Kristo. Moyo na nia huumbika upya kwa mfano wake atendaye kazi ndani yetu, ambaye huvihisha vyote chini yake. Halafu sheria ya Mungu huandikwa katika dhamiri zetu na roho zetu, nasi tunaweza kusema pamoja na Kristo, kwamba: “Kuyafanya mapenzi yako, ee Mungu, ndiyo furaha yangu.” Zaburi 40:8 TVV 92.5
Katika mazungumzo ya Yesu na Nikodemo, Yesu aliufunua mpango wa wokovu. Katika hotuba zake zote, hakuna hata moja ambayo alieleza mpango wa wokovu kwa ukamilifu hatua kwa hatua kazi inayopaswa kutendwa katika moyo wa mtu yeyote atakayeurithi ufalme wa mbinguni. Tangu mwanzo wa kazi yake, alieleza ukweli kamili kwa mbunge huyu wa Sanhedrin, ambaye ni mwalimu wa watu wa Israeli. Lakini viongozi wa Israel hawakuikubali nuru. Nikodemo alihifadhi kweli ya Mungu moyoni mwake, na kwa muda wa miaka mitatu matunda yalikuwa kidogo sana. TVV 93.1
Lakini maneno yaliyosemwa usiku katika mlima hayakupotea. Katika baraza la Sanhedrin Nikodemo alikazia kuuvunja mpango wa kumwangamiza Yesu. Mwishoni Yesu aliposulubishwa Nikodemo alikumbuka maneno ya Yesu kwamba “Kama Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele.” Nuru kutokana na maongezi ya usiku ilimulika msalabani pale Kalwari, na Nikodemo akamwona Yesu kuwa ndiye Mwokozi wa ulimwengu. TVV 93.2
Baada ya kufufuka kwake Bwana, wakati wanafunzi wametawanyika kwa ajili ya mateso. Nikodemo alijitokeza mbele. Alitumia mali yake kulisaidia kanisa, changa ambalo Wayahudi walikusudia kuliangamiza wakati wa kifo cha Kristo. Wakati wa hatari, Nikodemo aliyekuwa mwenye maswali na wasiwasi, alisimama imara kama mwamba, akiitetea imani na kulisaidia kahisa lipate kueneza Injili. Alitoa mali yote, akabaki kuwa maskini, lakini aliimarika katika imani aliyoipata wakati wa mazungunzo ya usiku. TVV 93.3
Nikodemo alihusiana na Yohana kwa damu kwa historia iliyosemwa, na kwa kalamu ya kuwafundisha watu mamilioni. Ukweli wanaofundisha leo ni muhimu kama ulivyokuwa wakati wa maongezi ya usiku, wakati mtu mkuu alipokuja kujifunza kwa mnyenyekevu wa Galilaya. TVV 93.4