Mamlaka na kanuni za imani ya Kanisa la Roma ziliachwa na Kanisa la Uingereza. Lakini taratibu nyingi za ibada hazikuachwa. Ilidaiwa kuwa mambo ambayo hayajakatazwa ndani ya Maandiko hayana asili ya uovu. Kuyashika kulielekea kupunguza umbali uliotenganisha kati ya makanisa ya matengenczo na Kanisa la Roma. Pia ilidaiwa kwamba yangewahamasisha wauamini wa Kanisa la Roma kuikubali imani ya Waprotestanti. TK 187.1
Kundi lingine halikufuata dhana hiyo. Wao waliona kuwa desturi hizo ni ishara za utumwa wa kule walikokuwa wamekombolewa. Walitoa sababu kuwa Mungu, ndani ya Neno lake ameweka taratibu zinazoongoza ibada yake, na kwamba wanadamu hawana uhuru wa kuziongea ama kuzipunguza. Kanisa la Roma lilianza kwa kuamuru mambo ambayo Mungu hakuyakataza, likamalizia kwa kukataza yale ambayo kwa wazi aliyaamuru. TK 187.2
Watu wengi waliziona desturi za Kanisa la Uingereza kama makumbusho ya ibada ya sanamu, na hawakujiunga katika ibada zake. Lakini kanisa likisaidiwa na mamlaka ya serikali halikuruhusu maoni tofauti. Mikusanyiko ya ibada isiyo na kibali ilipigwa marufuku kwa adhabu ya kifungo, kuhamishwa, au kifo. Watu walioitwa Puritans waliwindwa, waliteswa, na kufungwa gerezani; hawakuweza kugundua ahadi ya siku zilizo bora. Baadhi yao walipoamua kutafuta hifadhi huko Uholanzi, walisalitiwa na kutiwa mikononi mwa adui zao. Uvumilivu wa kudumu hatimaye ulishinda, na walipata hifadhi kwenye fukwe nzuri. TK 187.3
Walikuwa wameacha nyumba zao na njia za kupatia mahitaji yao. Walikuwa wageni kwenye nchi ya ugeni wakalazimika kuishia kwenye kazi za kubahatisha ili kupata riziki zao. Lakini hawakupoteza muda kwa uvivu na manung’uniko. Walimshukuru Mungu kwa ajili ya baraka alizowapa na wakapata furaha kwenye ushirika wa kiroho usio na usumbufu. TK 187.4