Kama ilivyokuwa kwa Mahujaji, Roger Williams alikuja kwenye Ulimwengu Mpya ili kufurahia uhuru wa kidini. Lakini, yeye, kinyume na wao, alikuwa ameona kile ambacho wachache sana walikuwa wamekiona-kwamba uhuru ni haki ya wote isiyoweza kuondolewa. Alikuwa mtafutaji wa dhati wa ukweli. Williams “alikuwa mtu wa kwanza katika ulimwengu wa Ukristo wa kisasa kuanzisha serikali ya kiraia yenye msingi wa fundisho la uhuru wa dhamiri.” 184Bancroft, pt. 1, ch.15, par. 16. “Umma au mahakimu wanaweza kuamua,” alisema, “iliyo haki kutoka mwanadamu hadi mwanadamu; lakini wanapojaribu kuamuru wajibu wa mwanadamu kwa Mungu, wametoka nje ya mstari, na hakutakuwa na usalama; maana ni wazi kuwa kama hakimu angekuwa na uwezo, leo angeweza kuamuru aina moja ya maoni au imani na kesho aina nyingine; kama ilivyofanywa na wafalme na malkia mbalimbali huko Uigereza na Mapapa na mabaraza mbalimbali ndani ya Kanisa la Roma.” 185Martyn, vol. 5, p. 340. TK 189.3
Mahudhurio kanisani yalikuwa yanalazimishwa kwa adhabu ya faini au kifungo. “Kuwalazimisha wanadamu waungane na wale wenye imani tofauti nao, Williams alichukulia kuwa ni ukiukaji wa wazi wa haki za asili; kuwakokota wasio na dini na wasio hiari hadi kwenye ibada ya hadhara, ilionekana tu kama kushurutisha unafiki... ‘Hakuna mtu apaswaye kulazimishwa kuabudu au kuendesha ibada kinyume na matakwa yake’” 186Bancroft, pt. 1, ch. 15, par. 2. TK 190.1
Roger Williams aliheshimiwa, lakini hitaji lake la uhuru wa kidini halikuweza kuvumiliwa. Ili kujiepusha asikamatwe alilazimika kutoroka katikati ya baridi na dhoruba za msimu wa baridi hadi kwenye msitu usiofikika. TK 190.2
Anasema, “Kwa majuma kumi na manne, nilikuwa nimetupwa pekee yangu kwenye kipindi kichungu, bila kujua mkate ama kitanda vilimaanisha nini.” Lakini “Kunguru walinilisha jangwani” na mti wenye uwazi mara zote ulitumika kama nyumba. 187Martyn, vol. 5, pp. 349, 350. Aliendelea na ukimbizi wake wenye uchungu kupitia kwenye barafu na msitu usio na njia hadi alipopata kimbilio kwenye kabila moja la Kihindi ambalo lilimwamini na kumpenda. TK 190.3
Aliweka msingi wa taifa la kwanza la kisasa ambalo lilitambua “kuwa kila mtu anatakiwa awe na uhuru wa kumwabudu Mungu kulingana na nuru ya dhamiri yake.” 188Ibid., vol. 5, p. 354. Taifa lake dogo la Rhode Island, liliendelea kukua na kustawi hadi misingi ya kanuni zake-uhuru wa kiraia na wa kidini-zilipokuwamisingi ya Jamhuri ya Marekani. TK 190.4