Katika kuitazamia siku ya Bwana Neno la Mungu linawaita watu wake kuutafuta uso wake kwa toba: Kwa maana siku ya Bwana inakuja. Kwa sababu inakaribia; Takaseni saumu, kusanyeni kusanyiko kuu; Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto, Na hao wanyonyao maziwa: . . . “Hao makuhani, wahudumu wa Bwana, na walie kati ya patakatifu na madhabahu” “nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea; rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.” Yoeli 2:1, 15-17, 12, 13. TK 199.4
Ilikuwa inatakiwa ifanyike Kazi kubwa ya Matengenezo ili kuwaandaa watu kusimama katika siku ya BWANA. Kwa rehema yake Mungu alikuwa anataka kutuma ujumbe... kuwaamsha watu wake wanaomkiri na kuwaongoza kujiandaa kwa ajili ya ujio wa BWANA. TK 199.5
Onyo hili linaonekana katika Ufunuo 14. Hapa kuna ujumbe wenye sehemu tatu unaowakilishwa ukitangazwa na malaika wa mbinguni na muda mfupi baadaye kufuatiwa na kuja kwa Mwana wa Adamu kuvuna “mavuno ya dunia.” Nabii alimwona malaika... “akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Ufunuo 14:6,7. TK 200.1
Ujumbe huu ni sehemu ya “Injili ya milele.” Kazi ya kuhubiri wamekabidhiwa wanadamu. Malaika watakatifu wanaelekeza, lakini kazi ya kuhubiri Injili inafanywa na watumishi Wakristo duniani. Watu waaminifu, ambao ni watiifu kwa uongozi wa Roho Mtakatifu wanaihesabu Injili kuwa ni, “bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.” “Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.” Mithali 3:14; Zaburi 25:14. TK 200.2