“Giza la mchana lilikuwa sio la kawaida lenye kutisha kuliko lile la usiku. Ingawa mwezi ulikuwa mpevu, hakuna kitu kilichokuwa kinaonekana isipokuwa kwa msaada wa kutumia mwanga, ambao wakati unaonekana kutoka kwenye nyumba za jirani na sehemu nyingine kutoka umbali mfupi ilionekana kama giza la Misri lililoonekana kutopitisha miali ya mwanga.” 196Isaiah Thomas, Massachusetts Spy; or, American Oracle of Liberty, vol.10, no. 472, (May 25, 1780). “Kama kila kitu cha angani kinachotoa mwanga katika ulimwengu kingefunikwa na vivuli visivyo pitisha mwanga au kuondolewa, giza lisingekuwa zito sana” 197Letter b Dr. Samuel Tenney, of Exter, New Hampshire, December 1785, in Massachussetts Historical Society Collections, 1792, (1st series, vol. 1, p. 97). Baada ya usiku wa manane giza lilitoweka, na mwezi ulipoonekana kwa mara ya kwanza, ulikuwa na rangi ya damu. TK 197.4
Tarehe 19 Mei 1780 inakumbukwa katika historia kama “siku ya giza.” Tangu enzi za Musa hakuna giza zito, lililofunika sehemu kubwa ya nchi, na lililochukua muda mrefu lililowahi kuwekwa kwenye kumbukumbu. Maelezo yaliyotolewa na mashahidi walioona kwa macho ni mwangwi wa maneno yaliyoandikwa na Yoeli miaka 2500 iliyopita. “Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla haijaja hiyo siku ya Bwana iliyo kuu na itishayo.” Yoeli 2:31. TK 198.1
“Basi mambo hayo yaanzapo kutokea,” Kristo alisema, “changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu, kwa kuwa ukombozi wenu umekaribia.” Akawaonesha mtini wanafunzi wake, “Wakati iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno yamekaribia. Nanyi kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu u karibu.” Luka 21:28, 30,31. TK 198.2
Lakini kanisani upendo kwa Kristo na imani katika ujio wake imepungua. Watu wanaokiri ni wa Mungu walipofushwa wasiyaelewe maelekezo ya Mwokozi kuhusu ishara ya kuja kwake. Fundisho la kuja kwa Yesu mara ya pili limepuuzwa, hadi kwa kiasi kikubwa lilipokuwa limepuuzwa na kuachwa hasa Marekani. Jitihada kubwa katika utafutaji wa pesa, kukimbilia umaarufu na madaraka kuliwafanya watu kuifikiria kwamba siku hiyo ya kutisha iko wakati ujao, utaratibu wa sasa wa mambo utakapokuwa umepita. TK 198.3
Mwokozi aliwatahadharisha mapema hali ya wale watakaorudi nyuma katika imani kabla ya kuja kwa Yesu mara ya pili. Kwa wale watakaokuwa hai wakati huo, ujumbe Wakristo ni: “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo; “Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.” Luka 21:34, 36. TK 199.1
Ilikuwa ni jambo la muhimu kwamba wanadamu waamshwe ili wajiandae kwa ajili ya matukio ya kutisha ya kufungwa kwa mlango wa rehema. TK 199.2
Siku ya Bwana ni kuu, yenye kitisho sana; naye ni nani awezaye kuistahimili? Ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye ambaye “uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu.” Na asiyeweza “kuangalia uovu?” “Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali.” “Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa” “Na huko utajiri wao utakuwa mateka, na nyumba zao zitakuwa ukiwa” Yoeli 2:11; Habakuki 1:13; Isaya 13:11; Sefania 1:18,13. TK 199.3