Miaka ishirini na mitano baadaye, ilionekana ishara nyingine iliyotajwa kwenye unabii-kutiwa giza kwa jua na mwezi. Wakati wa utimilifu wake ulikuwa umetajwa kwa usahihi katika mazungumzo ya Mwokozi akiwa na wanafiinzi wake kwenye mlima wa Mizeituni “Lakini siku zile, baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake.” Marko 13:24. Siku au miaka 1260 zilifikia mwisho wake mwaka 1798. Robo ya kame kabla, mateso yalikuwa yamekoma kabisa. Kufuatia mateso haya, jua lingetiwa giza. Siku ya tarehe 19 Mei 1780 unabii huu ulitimia. TK 196.2
Shahidi aliyeshuhudia kule Massachusetts analilielezea tukio kama ifuatavyo: “Wingu zito jeusi lilitanda katika anga lote isipokuwa ukingo mwembamba kwenye upeo wa macho, na kulikuwa na giza kama lile la saa 3 usiku wa majira ya joto . . . TK 196.3
“Woga, wasiwasi, na hofu iliamza kuingia katika akili za watu. Wanawake walisimama mlangoni wakiangilia nje kwenye sura ya nchi iliyofunikwa na giza; watu walirejea kutoka kwenye sehemu zao za kazi mashambani. Seremala aliacha vifaa vyake, Mfua chuma aliiacha karakana, Mfanyabiashara aliacha meza yake. Watoto wa shule waliruhusiwa kutawanyika kwenda nyumbani, nao kwa hofu walikimbia kwenda nyumbani. Wasafiri walijihifadhi kwenye nyumba za mashambani zilizokuwa karibu. “Ni nini kinachokuja?” kila mtu alikuwa anauliza. Ilionekana kana kwamba kimbunga kilikuwa kinakaribia kupita kwa kasi katika ardhi, au kana kwamba ilikuwa ni siku ya kuangamia kila kitu. TK 196.4
“Mishumaa ilitumika; na moto mkali uliwaka ukiwa na mwangaza mkubwa kama ule wa jioni isiyo na mbalamwezi katika kipindi cha kuputika. . . .Kuku walirudi kwenye mabanda yao na kulala, ngombe walirudi kwenye mabanda yao na kulala, vyura walitoa sauti zao, Ndege waliimba nyimbo zao za jioni, Popo walirukaruka. Lakini wanadamu walijua kwamba usiku haujafika. . TK 197.1
“Mikusanyiko ya watu katika sehemu . . . .nyingi ilikutana. Mafungu kwa ajili ya mahubiri ambayo yalikuwa hayajaandaliwa vizuri yalikuwa ni yale yale ya siku zote yaliokuwa yanaonesha kwamba giza liko kwenye unabii wa Biblia . . .Giza lilikuwa zito zaidi muda mfupi baada ya saa tano kamili.” 194The Essex Antiquarian, April 1899, vol. 3, no. 4, pp. 53, 54. TK 197.2
“Katika sehemu kubwa ya nchi, giza lilikuwa zito mno wakati mchana, kiasi kwamba watu hawakuweza kujua muda kwa kuangalia saa za mkononi au saa za ukutani wala hawakuweza kula au kufanya kazi zao za nyumbani, bila mwanga wa mshumaa.” 195William Gordon, Hisory of the Rise, Progress and Establishment of the Independence of the U.S.A., vol. 3, p. 57. TK 197.3