Kama utimilifu wa unabii huu, mwaka 1755, kulitokea tetemeko la kutisha zaidi kuwahi kuwekwa kwenye kumbukumbu. Linajulikana kama tetemeko la Lisbon, lilienea katika mabara ya Ulaya, Afrika, na Marekani. Tetemeko hilo lilitokea huko Greenland, visiwa vya West Indies, Madeira, Norway na Sweden, Uingereza na Ireland, na lilienea kwenye maili za mraba zisizopungua milioni 4. Katika Afrika nguvu yake ilikuwa sawa na ile iliyokuwa Ulaya. Sehemu kubwa ya nchi ya Algiers iliharibiwa. Wimbi la bahari lililochukua eneo kubwa liligharikisha pwani ya Hispania na Afrika na kuimeza miji. TK 195.3
Baadhi ya ile milima mikubwa ya Ureno, ilitikiswa kwa nguvu, kana kwamba ni kutoka kwenye misingi yake: na baadhi ya milima vilele vyake vilifunuka, kugawanyika na kuvunja vunjwa kwa namna ya ajabu, vifusi vyake vikubwa vilitupwa kwenye mabonde yaliyokuwa jirani. Inasemekana kuwa miali ya moto ilitokea katika milima hii. TK 195.4
Katika mji wa Lisbon, “Ngurumo ya radi ilisikika kutoka chini ya ardhi, na ghafla baadaye, mshindo mkuu uliitupa chini sehemu kubwa ya mji ule. Ndani ya dakika kama sita, watu wapatao elfu sitini walikuwa wameangamia. Bahari Kwanza bahari ilikupwa na kuacha nchi kavu; baadaye lilikuja wimbi lenye kimo cha futi hamsini au zaidi ya kimo chake cha kawaida.” 192 Sir Charles Lyell, Principles of Geology, p. 495. TK 195.5
“Tetemeko lilitokea mwisho wa juma, watu wakiwa wamejaa kwenye makanisa na nyumba za watawa, ni wachache sana kati yao walisalimika” 193Encyclopedia Americana, art. “Lisbon” (ed. 1831). “Hofu iliyowakumba watu ilikuwa haielezeki. Hakuna mtu aliyelia; ilikuwa ni zaidi ya machozi. Walikimbia huku na huko, wakiwa wamefadhaika kwa hofu na mshangao, wakipigapiga nyuso na vifua vyao nakulia ‘dunia imefika mwisho!’ Akina mama waliwasahau watoto wao, walizunguka wakikimbia wakiwa na misalaba yenye sanamu ya Yesu aliYesulubiwa. Kwa bahati mbaya wengi walikimbilia makanisani kwa ajili ya usalama; Sakramenti ilioneshwa lakini haikusaida, watu hawa maskini walikumbatia madhabahu; sanamu, mapadre, na watu walifunikwa katika maangamizi hayo ya jumla.” TK 196.1