Ahadi ya kuja kwa Kristo mara ya pili kukamilisha kazi kubwa ya ukombozi ni wazo kuu la Maandiko Matakatifu. Tangu Bustani ya Edeni, wana wa imani wamekuwa wakingojea kuja kwake Yeye Aliyeahidiwa kuwarejeshea Paradiso iliyokuwa imepotea. TK 193.1
Henoko mtu wa saba kutoka kwa kwao waliokuwa wanaishi Edeni, ambaye alitembea na Mungu kwa kame tatu anasema, “Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, ili afanye hukumu juu ya watu wote.” Katika usiku wa maumivu makali Ayubu alipaza sauti yake na kusema, “Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi:...Lakini, pasipokuwa na mwili wangu nitamwona Mungu; Nami nitamwona mimi nafsi yangu, na macho yangu yatamtazama, wala si mwingine.” Ayubu 19:25-27. Washairi na manabii wa Biblia wameelezea sana habari za kuja kwa Kristo kwa maneno yenye kuvutia sana. “Mbingu na zifurahi na nchi ishangilie, ...mbele za Bwana: kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja ili aihukumu nchi: Atauhukumu ulimwengu kwa haki.” Zaburi 96:11-13. TK 193.2
Isaya anasema: Na katika siku hiyo watasema, Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.” Isaya 25:9. TK 193.3
Kipindi kile Mwokozi alipokaribia kutenganishwa na wafuasi wake, aliwafariji kwa huzuni waliyokuwa nayo kwa kuwathibitishia kwamba atakuja tena: “Msifadhaike mioyoni mwenu; ...maana naenda TK 193.4
kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda...nitakuja tena niwakaribishe kwangu.” “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake; na mataifa yote watakusanyika mbele zake” Yn. 14:2, 3; 25:31,32. TK 193.5
Malaika walimdia kuwaambia wanafunzi juu ya ahadi ya kumdi kwake: “Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.” Mdo. 1:11. Na Paulo anashuhudia: “Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu” 1 Wathesalonoke 4:16. Nabii wa Patmo anasema: “Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona” Ufu. 1: 7. TK 193.6
Kanuni ya muda mrefu ya uovu itakomeshwa: “Ufalme wa dunia” umekwisha kuwa “ufalme wa Bwana wetu na Wakristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.” Ufu. 11:5. “Bwana MUNGU atakavyootesha haki na sifa mbele ya mataifa yote.” Isaya 61:11. TK 194.1
Ufalme wa amani wa Masihi utaanzishwa: “Maana Bwana ameufariji Sayuni; amepafariji mahali pake palipokuwa ukiwa; amefanya jangwa lake kuwa kama bustani ya Edeni, na nyika yake kama bustani ya Bwana.” Isaya 51:3. TK 194.2
Kuja kwa Bwana limekuwa ni tumaini la wafuasi wake wa kweli kwa vizazi vyote. Katikati ya maumivu na mateso, “mafunuo ya Mungu mkuu na Mwokozi wetu” limekuwa ni “tumaini lenye baraka” Tito 2:13. Paulo alikuwa analenga tukio la ufufuo utakaoambatana na kuja kwa Mwokozi, wakati wale waliokufa katika Kristo watafufuka, wataungana na walio hai na kisha kunyakuliwa ili wakutane na Bwana hewami. “Kwa hiyo,” alisema, “farijianeni kwa maneno hayo” 1 Wathesalonoke 4:17. TK 194.3
Katika kisiwa cha Patmo Mwanafunzi mpendwa alisikia ahadi kwamba, “Naam; naja upesi.” Na mwitikio wake unawakilisha ombi la kanisa, “na uje, Bwana Yesu.” Ufunuo 22:20. TK 194.4
Kutoka kwenye gereza la chini ya ardhi, kwenye mti na mbele ya jukwaa la kuchomea watu moto, mahali ambapo watakatifu na wafiadini waliushuhudia ukweli, yalitoka maneno ya imani na tumaini lao kwa kame nyingi. Mmoja kati ya Wakristo hawa alisema, “Wakiwa na uhakika juu ya kufufuka kwake, na kisha ufufuo wao wenyewe Yeye atakapokuja, kwa ajili ya hili; walikidharau kifo, na walionekana kuwa wako juu ya kifo.” 191Daniel T. Taylor, The Reign of Christ on Earth: or, The Voice of the Church in All Ages, p. 33. TK 194.5
Watu waliokuwa wanaitwa Waldensia waliidumisha imani hiyo hiyo. Wycliffe, Luther, Calvin, Knox, Ridley, na Baxter walitazamia kwa imani kuja kwa Bwana. Hilo pia lilikuwa ni tumaini la kanisa la mitume, tumaini la “kanisa la jangwani”, na lile la Wanamatengenezo. TK 195.1
Unabii hautabiri tu namna na kusudi la kuja kwa Kristo, lakini unaonesha ishara zitakazowajulisha watu kwamba ile siku imekaribia. “kutakuwa na ishara katika jua, na mwezi, na nyota” Luka 21:25. “jua litatiwa giza, na mwezi hatautoa mwanga wake. na nyota za mbinguni zitakuwa zinaanguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika. Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu nyingi na utukufu.” Marko 13:24-26. Hivi ndivyo Yohana wa Ufunuo alivyoielezea ishara ya kwanza kati zile zitakazotangulia kuja kwake mara ya pili: “palikuwa na tetemeko kuu la nchi; jua likawa jeusi kama gunia la singa, mwezi wote ukawa kama damu.” TK 195.2