Mkulima mnyofu na mwaminifu ambaye alikusudia kuujua ukweli alikuwa ni mtu aliyechaguliwa na Mungu kuongoza utangazaji wa kurudi kwa Yesu mara ya pili. Kama wanamatengenezo wengine wengi, William Miller alipambana na umaskini na alijifunza somo la kujinyima na kujikana nafsi TK 204.1
Hata katika wakati wa utoto wake alionesha ushahidi usio wa kawaida wa akili yenye uwezo katika utendaji. Alipokuwa mtu mzima akili yake ilikuwa na uwezo na maendeleo na alikuwa na hamu kubwa ya kujua maarifa. Kupenda kwake kujifunza na tabia ya kuwa mwangalifu katika kufikiri na kupima mambo kulimfanya awe na uamuzi sahihi na mtazamo sahihi. Alikuwa mwenye tabia nzuri kiroho na sifa njema kwa watu. Alipata sifa katika ofisi za kiraia na kijeshi. Utajiri na heshima vilionekana kuwa tayari kwa ajili yake.. TK 204.2
Wakati wa utoto wake, alikuwa na uelekeo wa kuvutiwa na mambo ya dini. Hata hivyo mwanzoni mwa utu uzima aliingizwa kwenye chama cha deists (Yaani wanaoamini kuwepo Mungu mwumbaji lakini asiyejishughulisha na viumbe wake), watu ambao mvuto wao ulikuwa mkubwa maana wengi wao walikuwa raia wema wenye ubinadamu na wakarimu.. Wakiwa wanaishi kwenye taasisi za Kikristo, kwa kiasi fulani tabia zao zilikuwa zimeathiriwa na mazingira yao. Sifa njema zilizowajengea heshima, zilitokana na Biblia na lakini vipawa hivyo vizuri, vilipotoshwa na kuwa na ushwishi uliokuwa kinyume na Neno la Mungu. Miller aliongozwa kufuata mitazamo yao. TK 204.3
Fasili za Maandiko za wakati huo zilileta ugumu ambao kwake ulioelekea kutoondosheka: akiweka kando Biblia, bado imani yake mpya, , haikuleta kitu chochote bora, na alibaki katika hali ya kutoridhika. Lakini Miller alipokuwa na umri wa miaka 34, Roho Mtakatifu aliushawishi moyo wake juu ya hali yake ya dhambi. Hakuwa na uhakika wa furaha baada ya kifo. Mustakabali ulikuwa giza na wakuhuzunisha. Akirejea katka hisia alizokuwa nazo kipindi hiki, alisema: TK 204.4
“Mbingu zilikuwa kama shaba juu ya kichwa changu na dunia kama chuma miguuni pangu...Kwa Kadiri nilivyofikiri zaidi, ndivyo uamuzi wangu ulivyozidi kukosa umakini. Nilijaribu kuacha kufikiri, lakini sikuweza kuyadhibiti mawazo yangu. Kwa hakika nilihuzunika, lakini sikuelewa chanzo chake. Nilinung’unika na kulalamika lakini, sikujua ni kwa nani nilifanya hivyo. Nilijua kuwa kulikuwa na kosa, lakini sikujua ni kwa namna gani ama ni wapi kwa kuupata ukweli.” TK 205.1