“Ghafla” alisema, “tabia ya Mwokozi kwa dhahiri ilitia mvuto akilini mwangu”. Ilionekana kuwa yupo Aliye bora na mwenye huruma kiasi cha yeye mwenyewe kulipia kosa la dhambi zetu na hivyo kutuokoa katika mateso na adhabu ya dhambi ... lakini swali liliibuka, inawezekanaje kuthibitika kwamba huyo yupo? Niligundua kuwa bila Biblia nisingeweza kupata ushahidi wa uwepo wa Mwokozi kama huyo, au ushahidi wa hali ya baadaye. TK 205.2
“Niliona kuwa Biblia ilikuwa inamdhihirishaMwokozi yule yule nilikuwa ninamhitaji; nilishangaa kuwa kitabu kisichovuviwa kingewezaje kuelezea kanuni zinazokidhi kikamilifu kwa kiasi hicho endana mahitaji ya ulimwengu ulioanguka. Ilinibidi kukubali kwamba Maandiko lazima uwe ni ufunuo kutoka kwa Mungu. Maandiko yakawa ndiyo furaha yangu; nilimpata rafiki Yesu. Mwokozi, kwangu akawa mkuu miongoni mwa elfu kumi; na Maandiko ambayo mwanzo yalikuwa giza na yenye kukinzana, sasa yakawa taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu .. Nilimpata Bwana Mungu kuwa mwamba katikati ya bahari ya maisha. Biblia ikawa kitabu changu kikuu cha mafunzo, na ninaweza kusema , niliichuguza kwa furaha kuu... nilistaajabu kwa nini nilikuwa sijauiona uzuri na utukufu wake hapo kabla, nikashangaa kuwa ningewezaje kuikataa nilipoteza hamu yote ya vitabu vingine na nilielekeza moyo wangu kupata hekima kwa Mungu” 198S. Bliss, Memories of William Miller, pp. 65-67 TK 205.3
Miller alikiri imani yake hadharani. Lakini wenzi wake wasioamini walitanguliza hoja zote ambazo yeye mwenyewe mara kwa mara alizipinga kwa kutumia Maandiko. Aliionesha mantiki ya kuwa kama Biblia ni ufunuo kutoka kwa Mungu, ni lazima ikubaliane yenyewe. Aliazimu kujifunza Maandiko na kupata uhakika endapo kila ukinzani uliokuwa dhahiri ungeweza kupatanishwa. TK 206.1
Bila kutumia vitabu vya ufafanuzi wa Biblia alilinganisha andiko na andiko kwa msaada wa maelezo ya pembeni na itifaki. Alianza na kitabu cha Mwanzo akasoma mstari mmoja baada ya mwingine, alipogundua kitu chochote chenye ugumu,ilikuwa ni desturi yake kukilinganisha na kila fungu lingine lililoelekea kurejeza kwenye mada inayohusika. Kila neno lilipewa uzito wake ndani ya fungu. Kwa hiyo wakati wowote alipokutana na aya ngumu kueleweka alitafuta maelezo kwenye sehemu nyingine za Maandiko. Alijufunza kwa maombi ya dhati ili apate ufahamu kutoka mbinguni, na akaupata uzoefu wa ukweli wa maneno ya mtunga zaburi kuwa: “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.” Zaburi 119:130. TK 206.2
Alijifunza vitabu vya Danieli na Ufunuo kwa shauku kubwa na akagundua kuwa vielelezo vya vingeweza kueleweka. Aliona kuwa vielelezo vyote, sitiari, tashbihi, nk., vilikuwa vimeelezewa pale pale au vimefafanuliwa kwenye Maandiko mengine na vingeweza kueleweka neno kwa neno. Kiungo kimoja baada ya kingine katika mnyororo wa ukweli kilifanya jitihada yake kuwa na faida. Hatua kwa hatua alizifuatilia njia kuu za unabii. Malaika wa mbinguni waliongoza fikra zake. TK 206.3
Miller aliridhika kuwa mtazamo wa wengi kwamba kutakuwa na milenia ya muda mfupi kabla ya mwisho wa dunia haujengwi katika Neno la Mungu. Fundisho hili, linaloelekeza kwenye miaka elfu moja ya amani kabla ya kuja kwa Bwana, ni kinyume na mafundisho ya Kristo na mitume wake, ambao walitamka kwamba sharti ngano na magugu vikue pamoja hadi wakati wa mavuno, mwisho wa dunia, na kwamba “watu wabaya na wadanganyaji wataendelea, na kuzidi kuwa waovu.”2Timotheo 3:13. TK 206.4