Go to full page →

Tofauti na Fasili za Wengi TK 228

Wolff aliandika hivi juu ya mfumo wa kufasili Maandiko uliokuwa unatumiwa na wengi, “Sehemu kubwa ya Kanisa la Kikristo imechepuka kutoka katika maana sahili ya Biblia, na ...kudhani wanaposoma Wayahudi ni lazima waelewe Watu wa Mataifa; na wanaposoma TK 228.4

Yerusalemu, ni lazima waelewe kanisa; na kama ikisemwa dunia, inamaanisha anga; na kuja kwa Bwana, ni lazima waelewe maendeleo ya vyama vya kimisionari; na kwenda katika mlima wa nyumba ya Bwana, inamaanisha mkutano wa Wamethodisti mashuhuri. “ 211Joumal of the Rcv. Joseph Wolff, p. 96. TK 229.1

Tangu mwaka 1821 hadi 1845, Wolff alisafiri kule Misri, Ethiopia, Palestina, Shamu, Uajemi, Bokhara, India, na Marekani. TK 229.2