Dk. Wolff alitembelea nchi nyingi za watu wakatili kabisa bila ulinzi wo wote; akistahimili matatizo na kuzungukwa na hatari nyingi. Alikosa chakula, akauzwa kama mtumwa, akahukumiwa kifo mara tatu, akazingirwa na wanyang’anyi, na wakati mwingine alinusurika kufa kwa sababu ya kiu. Wakati fulani alivuliwa na kuachwa atembee kwa miguu mamia ya kilometa katika milima, wakati theluji ikipiga uso wake na miguu yake iliyokuwa peku ikifa ganzi kwa sababu ya ardhi iliyokuwa imeganda. TK 229.3
Alipoonywa asisafiri bila ulinzi katika ya makabila katili, alisema kuwa amepewa silaha—“maombi, ari kwa ajili ya Kristo, na imani kubwa kuhusu aliye msaada wake.” “Pia nimepewa upendo kwa ajili ya Mungu na jirani yangu katika moyo wangu, na Biblia iko mkononi mwangu.” “Nilikuwa naona kuwa nguvu yangu ilikuwa katika Kitabu, na kwamba uwezo wake ungenihifadhi.” 212W. H. D. Adams, In Perils Oft, pp. 192, 201. TK 229.4
Alisonga mbele hadi ujumbe ulipoenea katika sehemu kubwa ya ulimwengu uliokuwa na wakazi. Alieneza neno la Mungu katika Iugha mbali mbali kwa Wayahudi, Waturuki, Waparsi, Wahindu na mataifa mengine pamoja na jamii zingine, na kila mahali alitangaza kukaribia kwa ujio wa Masihi. TK 229.5
Kule Bokhara alikuta fundisho la kuja kwa Bwana hivi karibuni likishikiliwa na watu waliotawanyika. Anasema, Waarabu wa Yemeni, “wana kitabu kiitwacho Seera kinachozungumzia kuja kwa Kristo na utawala wake wa utukufu; na wanatarajia matukio makubwa katika mwaka 1840.” “Niliwakuta wana wa Israeli, wa kabila la Dani, ... pamoja na Warekabi... wanaotarajia kuja upesi kwa Masihi akiwa katika mawingu ya mbinguni.” 213Joumal of the Rev. Joseph Wolff, pp. 377, 389. TK 229.6
Imani kama hiyo ilikutwa na mmisionari mwingine huko Tatar. Kuhani wa Tatar aliuliza Yesu atarudi lini. Mmisionari huyo aliposema hajui lo lote, yule kuhani alishangazwa na ujinga huo kwa mwalimu huyu wa Biblia, naye akamwelezea imani aliyokuwa nayo, iliyokuwa inatokana na unabii, kwamba Kristo angekuja manamo mwaka 1844. TK 230.1