Lakini tena, muda uliotarajiwa ulipita, na Mwokozi wao hakutokea. Sasa walijisikia kama Mariamu alivyojisikia alipofika kwenye kaburi la Mwokozi na kukukuta liko tupu, ambaye alisema akilia: “wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka.” Yohana 20:13. TK 252.2
Wasiwasi kwamba ujumbe huo ungeweza kuwa wa kweli, ulisaidia kuwafanya wasioamini wanyamaze. Lakini dalili za ghadhabu ya Mungu zilipokosekana, walizinduka kutoka katika wasiwasi wao na kuanza tena dhihaka na kejeli zao. Sehemu kubwa ya wale waliokuwa wamekiri kuamini waliikana imani. Wenye kudhihaki waliwapata walio dhaifu na waoga na kuwavutia upande wao, na hawa wote waliungana katika kutangaza kwamba dunia ingeweza kubakia hivyo kwa niaka elfu. TK 252.3
Wale waumini wanyofu walikuwa wameacha vyote kwa ajili ya Kristo, na kwa kuamini kwao, walikuwa wameshatoa onyo la mwisho kwa ulimwengu. Walikuwa wamemwomba Mungu kwa shauku kubwa, “Na uje Bwana Yesu.” Lakini sasa kurudia tena mahangaiko ya maisha na kustahimili kejeli za wenye kudhihaki, lilikuwa jaribu kubwa. TK 252.4
Wakati Yesu alipoingia Yerusalemu kama mshindi, wafuasi wake waliamini kuwa alikuwa anakaribia kuketi kwenye kiti cha enzi cha Daudi na kuwakomboa Israeli kutoka kwa watesi wao. Wengi walitandika mavazi yao kama zulia katika njia yake au kutandaza matawi ya mitende kwa matumaini. Wanafunzi hao walikuwa wanatimiza makusudi ya Mungu, lakini walikuwa wanaelekea katika kuvunjika moyo sana. Siku chache baadaye walishuhudia Mwokozi wao akipiga kite wakati anakabiliana na mauti na wakamzika kaburini. Matumani yao juu ya Yesu yalikufa. Mpaka Bwana wao alipotoka kaburini ndipo walipoelewa kwamba yote yalikuwa yametabiriwa katika unabii. TK 253.1