Katika kipindi kirefu cha utawala wa Papa, walikuwepo mashahidi wa Mungu ambao walikuwa wanaithamini imani kwa Kristo kama mpatanishi pekee kati ya Mungu na wanadamu. Walikuwa wanaiamini Biblia kama kanuni pekee ya maisha, na kuitakasa Sabato ya kweli. Walikuwa wakiitwa waasi, maandishi yao yalipigwa marufuku, yakapotoshwa na kukataliwa. Lakini bado walisimama imara. TK 43.1
Hawa hawatajwi sana katika kumbukumbu za wanadamu, isipokuwa katika tuhuma kutoka kwa watesi wao. Kanisa la Roma lilikuwa linataka kungamiza kila ambacho lilikuwa linaona kuwa ni “uasi,” kiwe ni watu au maandishi. Kanisa la Roma pia liliamua kuharibu kumbukumbu zote za ukatili wake dhidi ya wale waliokuwa na maoni tofauti. Kabla ya kugunduliwa kwa elimu ya uchapaji, vitabu vilikuwa vichache; kwa hiyo kulikuwa hakuna jambo la kulizuia kanisa kutimiza makusudi yake. Mara baada ya utawala wa Papa kupata madaraka lilianza kuwaangamiza wote waliokuwa hawataki kukubaliana na utawala wake. TK 43.2
Katika nchi ya Uingereza, Ukristo wa kale ulikuwa umeota mizizi mapema, bila kuchafuliwa na uasi wa Kanisa la Roma. Zawadi pekee ambayo makanisa ya mwanzo ya Uingereza yalipata kutoka Rumi ni mateso toka kwa wafalme wa kipagani. Wakristo wengi waliokuwa wanakimbia mateso kule Uingereza walipata hifadhi kule Scotland. Toka huko ukweli ulipelekwa Ireland, na katika nchi hizi, ulipokelewa kwa furaha. TK 43.3
Watu wa Saxony walipovamia Uingereza, upagani ulipata nguvu, na Wakristo walilazimika kukimbilia milimani. Kule Scotland, kame moja baadaye, num iling’aa kwenda nchi za mbali. Toka Ireland, alikuja Columba na wafanyakazi wenzake, ambao walikifanya kisiwa cha Iona, kilichokuwa ukiwa, kuwa kituo cha kazi yao ya umisionari. Miongoni mwa walnjilisti hawa alikuwepo mshika Sabato ya kwenye Biblia, na kwa namna hiyo ukweli huu ulifikishwa kwa watu. Huko Iona ilianzishwa shule ambayo ilitoa wamisionari kwenda Scotland, Uingereza, Ujerumani, Uswisi na hata Italia. TK 43.4