Lakini Kanisa la Roma liliazimu kuiweka Uingereza chini ya utawala wake. Katika kame ya sita wamisionari wa Kanisa la Roma walianza kuwaongoa watu wa Saxony waliokuwa wapagani. Kazi ilipoendelea, viongozi wa utawala wa Papa walipambana na Wakristo wa kale-watu wa kawaida, wanyenyekevu na wenye tabia zilizojengwa kwenye Maandiko, mafundisho na uungwana. Viongozi wa Kanisa la Roma walionesha mapokeo potovu, majivuno na kiburi cha utawala wa Papa. Kanisa la Roma lilikuwa linataka makanisa haya ya Kikristo yamtambue Papa. Waingereza walijibu kwamba Papa hakuwa anastahili ukuu katika kanisa na walikuwa wanaweza kumpa heshima anayostahili kila mfuasi Wakristo. Walikuwa hawamjui Bwana mwingine isipokuWakristo. TK 44.1
Sasa roho ya kweli ya utawala wa Papa ilidhihirika. Kiongozi wa Kirumi akasema: “Kama hamtawapokea ndugu watakaowaletea amani, basi mtapokea maadui watakaowaletea vita.” 5J.H Merle D’ Aubigne, History of the Reformation of the Sbcteenth Century, kit. 17 sura ya 2. Vita na udanganyifu vilitumika dhidi ya mashahidi hawa wa imani ya Biblia, hadi makanisa ya Uingereza yalipoharibiwa na kulazimishwa kumtii Papa. TK 44.2
Katika nchi zilizokuwa nje ya utawala kwa Kanisa la Roma, jumuiya za Kikristo zilibaki zikiwa hazijaguswa sana na uchafu wa Kanisa la Roma. Waliendelea kuichukulia Biblia kama kanuni ya pekee ya imani. Wakristo hawa walikuwa wanaamini kuwa sheria ya Mungu ni ya milele na walikuwa wanaishika Sabato ya amri ya nne. Makanisa yaliyokuwa yanashika imani na desturi hizi yalikuwa Afrika ya Kati na miongoni mwa Waarmenia wa Asia. TK 44.3
Wawaldensia walikuwa mstari wa mbele kati ya wale waliokuwa wanapinga mamlaka ya Papa. Makanisa ya Piedmont yalidumisha uhuru wao katika nchi ambayo utawala wa Papa ulikuwa umeweka kiti chake. Lakini wakati ulifika ambapo Kanisa la Roma lilisisitiza kuwa makanisa hayo yajisalimishe. Hata hivyo, baadhi, walikataa kumtii Papa au maaskofu, wakiwa wameazimu kuhifadhi usafi na usahili wa imani yao. Kulitokea utengano. Wale waliokuwa wameshika imani ya kale sasa walijitoa. Baadhi yao wakiiacha milima yao ya Alps, waliinua bendera ya ukweli katika nchi za ugenini. Wengine walikimbilia katika maficho ya miamba ya milimani na huko waliendeleza uhuru wao wa kumwabudu Mungu. TK 44.4
Imani yao ya kidini ilikuwa imejengwa kwenye Neno la Mungu. Wakulima hao wa hali ya chini, waliokuwa wametengwa na dunia, hawakugundua wao wenyewe ukweli uliokuwa kinyume na mafundisho ya kanisa lililokuwa limeasi. Imani yao ya kidini ilikuwa ni urithi kutoka kwa baba zao. Walikuwa wanapigania imani ya kanisa la mitume. “Kanisa la jangwani” ndilo lililokuwa kanisa la kweli la Kristo, linalohifadhi hazina ya ukweli ambao Mungu aliwakabidhi watu wake waupeleke kwa ulimwengu, na siyo ule utawala wenye kiburi uliokuwa umetawazwa katika makao makuu ya dunia. TK 45.1
Miongoni mwa sababu kubwa zilizosababisha kujitenga kwa kanisa la kweli na Kanisa la Roma, ni chuki ya Kanisa la Roma dhidi ya Sabato ya Biblia. Kama ilivyotabiriwa katika unabii, mamlaka ya Papa iliikanyaga sheria ya Mungu. Makanisa yaliyokuwa chini ya Papa yalishurutishwa kuiheshimu Jumapili. Wakati uovu huo uliokuwa unaenea ukiendelea, wengi kati ya watu waaminifu wa Mungu walitatizwa kiasi kwamba walikuwa wakiiadhimisha Sabato, na Jumapili waliacha kufanya kazi. Lakini jambo hili halikuwaridhisha viongozi wa Kanisa la Roma. Walitaka Sabato inajisiwe, na waliwalaumu wale waliokuwa wanajaribu kuiheshimu. TK 45.2
Mamia ya miaka kabla ya kipindi cha matengenezo, Wawaldensia walikuwa na Biblia zilizokuwa katika lugha yao ya asili. Jambo hili liliwafanya wawe walengwa maalum ya mateso. Walilibainisha Kanisa la Roma kuwa ndiyo Babeli iliyoasi inayotajwa katika unabii. Walisimama imara kupinga uchafu wa ufisadi wa Kanisa la Roma, huku wakihatarisha maisha yao. Katika enzi zote za uasi, kulikuwa na Wawaldensia waliokuwa wanapinga ukuu wa Kanisa la Roma, waliokuwa wanapinga ibada ya sanamu, na waliokuwa wanashika Sabato. (Angalia kiambatisho). TK 45.3
Wawaldensia walipata mahali pa kujificha nyuma ya milima mirefu. Wakimbizi hawa waaminifu waliwaonesha watoto wao vilele vilivyokuwa vimeinuka juu katika utukufu na kuwaeleza juu ya yule ambaye Neno lakc linadumu kama milima ya milele. Mungu alikuwa ameweka milima imara; hakuna mkono ambao ungeweza kuiondoa isipokuwa wa yule aliye na uwezo usio na ukomo. Hivyo ndiyo alivyokuwa wamcisimika sheria yake. Mkono wa mtu usingeweza kubadili kipengele kimoja cha sheria ya Mungu kama vile usivyoweza kung’oa milima na kuitupa baharini. Wakimbizi hao hawakuendekeza huzuni kwa sababu ya ugumu wa maisha waliyokuwa wakipitia; hawakuwahi kuwa wapweke katika sehemu zilizojitcnga za milimani. Waliufurahia uhuru wao wa kuabudu. Waliimba nyimbo za sifa wakiwa katika majabali marefu, wala majeshi ya dola ya Kirumi hayakuweza kunyamazisha nyimbo zao za shukurani. TK 45.4