U Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake. Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya maShetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;. . . Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake. “Ufunuo 18:1,2,4. TK 364.1
Tangazo lililotolewa na malaika wa pili wa ufunuo 14 (fungu la 8) litarudiwa na kutaja maovu ambayo yamekuwa yakiingia Babeli tangu ujumbe huo ilipotolewa mwanzoni. TK 364.2
Hali mbaya inaelezwa hapa. Kwa kila ukataaaji wa ukweli akili za watu zinatiwa giza, mioyo yao ikiwa migumu zaidi. Wataendelea kukanyaga moja ya kanuni za Amri Kumi mpaka kuflkia hatua ya kuwatesa wale wanaoiamini kanuni hiyo kuwa ni takatifu. Kristo anaonekana kwamba sio kitu kwa sababu ya kudharau Neno lake na watu wake. TK 364.3
Kudai kuwa na dini kutatumika kama pazia la kufunika maovu. Imani ya mizimu inafungua mlango kukaribisha mafundisho ya Shetani na kwa hiyo mvuto wa malaika waovu utaonekana makanisani. Babeli amejaza kipimo cha hatia yake, na uharibifu unakaribia kutokea. TK 364.4
Lakini Mungu bado anao watu katika Babeli na waaminifu hawa ni lazima waitwe ili “wasishiriki dhambi zake na kupokea mapigo yake.” Malaika atashuka kutoka mbinguni akiiangazia dunia utukufu wake na kutangaza dhambi za Babeli. Mmwito utasikika, “tokeni kwake watu wangu” matangazo haya yana beba onyo la mwisho litakalotolewa kwa watu wa dunia. TK 364.5
Nguvu za dunia zikiungana katika vita dhidi ya amri za Mungu zitatangaza kwamba, “wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa” Ufunuo 13:16. Watazifuata tamaduni za kanisa kwa kuitunza sabato ya uongo. Wale wote watakaokataa hatimaye watatangaziwa kustahili amri ya kifo. Kwa upande mwingine sheria ya Mungu inayojumuisha siku ya Bwana ya kupumzika inatishia ghadhabu dhidi ya wale wote wanaoasi maagizo yake. TK 364.6
Kwa mambo ambayo yameelezwa bayana, yeyote atakayeikanyaga sheria ya Mungu na kuyatii maagizo ya wanadamu atapokea alama ya mnyama, ishara ya utii kwa mamlaka achaguayo kuitii badala ya Mungu. “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake.” Ufiinuo 14:9,10 TK 365.1
Hakuna hata mmoja atakayetaabika kwa ghadhabu ya Mungu mpaka pale ukweli utakapokuwa umeeleweka akilini mwake na dhamiri yake imeukataa. Wengi hawajapata fursa ya kusikiliza ujumbe wa pekee wa wakati huu. Yeye asomaye moyo wa kila mtu hatamwacha yeyote aliye na shauku ya ukweli adanganyike katika masuala ya pambano kuu. Kila mmoja atapkuwa na nuru ya kutosha ili afanye uamuzi wake kwa busara. TK 365.2