Sabato, jaribu kuu la uaminifu, ni ukweli ambao kwa nanma ya pekee unakanushwa. Wakati ushikaji wa sabato ya uongo utakuwa ndicho kiapo cha uaminifu kwa mamlaka inayopingana na Mungu; ushikaji wa Sabato ya kweli ni ushahidi wa utiifu kwa Muumbaji. Wakati ambapo kundi moja la watu linapokea alama ya mnyama lingine linapokea muhuri wa Mungu. TK 365.3
Utabiri anaonesha kwamba kutovumiliana katika mambo ya kidini kutatawala, kwamba kanisa na serikali vitawatesa wale wanaozishika amri za Mungu; umetamkwa kuwa hauna msingi na ni upuzi.. Lakini ushikajiwa Jumapili unavyoendelea kubishaniwa pote, tukio ambalo kwa muda mrefu limetiliwa shaka linaonekana kukaribia, ujumbe utakuwa na matokeo ambayo usingekuwa nayo hapo kabla. TK 365.4
Katika kila kizazi Mungu ametuma watumishi wake kukemea dhambi duniani na kanisani. Wanamatengenezo wengi walipokuwa wakianza kazi yao waliazimia kuwa na hadhari katika kushambulia dhambi za kanisa na za taifa. Walitumaini kwamba kwa kuwa kielelezo cha maisha safi ya Ukristo watawaongoza watu wairejee Biblia. Lakini Roho wa Mungu alikuja juu yao; pasipo kuogopa matatizo hawakuacha kuhubiri mafundisho yaliyo wazi ya Biblia. TK 365.5
Kwa hiyo ujumbe utahubiriwa. Mungu atatenda kazi kwa kutumia vyombo duni ambavyo vimejiweka wakfu kwa ajili ya huduma yake. Watenda kazi watakamilishwa kwa kupakwa mafuta na Roho Mtakatifu kuliko mafunzo ya taasisi za masomo. Watu watahamasika kwenda kazini wakiwa na ari takatifu wakitamka maneno ambayo Mungu amewapatia. Dhambi za Babeli zitawekwa wazi. Watu watachochewa. Maelfu hawajawahi kusikia maneno kama haya. Babeli ni kanisa lililoanguka kwa sababu ya dhambi zake, kwa sababu ya kuupuzia ukweli. Kama vile watu waendavyo kwa walimu wao wakiwa na swali kwamba “Je, mambo haya ndivyo yalivyo?” wachungaji watawajibu kwa kuwaeleza hadithi za uongo ili kuzinyamazisha roho zaozilizoamshwa. Lakini kwa sababu wengi wanadai andiko lililowazi kwamba “hivi ndivyo asemavyo Bwana,” huduma inayopendwa itawachochea watu wengi wanaopenda dhambi kuwakosoa na kuwatesa wale wanaoihubiri Injili hiyo. TK 366.1
Viongozi wa dini wataweka jitihada zisizo za kawaida ili kuuzuia ukweli, kupinga mjadala wa maswali haya muhimu. Kanisa litaomba msaada wa mkono wenye nguvu wa mamlaka za kiraia na katika kazi hii wafuasi wa Papa na Waprotestanti wataungana. Kadiri harakati za kulazimisha ibada ya Jumapili zinavyozidi kuwa imara, washika amri watatishiwa kwa kulipishwa faini na kufungwa magerezani. Baadhi wataahidiwa kupewa vyeo vya mvuto na zawadi nyingine ili wazikane imani zao. Lakini jibu lao litakuwa “tuoneshe kutoka kwenye Neno la Mungu kosa letu.” Wale watakaoshtakiwa mahakamani kufanya udhihirisho wenye nguvu wa ukweli, na baadhi wanaowasikia wataongozwa kufanya uamuzi wao wa kuzishika amri zote za Mungu. Vinginevyo maelfu hawatajua chochote kuhusu ukweli huu. TK 366.2
Utii kwa Mungu utachukuliwa kuwa ni kuasi. Wazazi watakuwa wakali kwa watoto wanaoamini. Watoto hawatapewa urithi na watafukuzwa nyumbani. “Wale wote watakao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.” . . 2 Timotheo 3; 12. Kadrii watetezi wa ukweli watakavyozidi kuikataa Jumapili, baadhi yao watatupwa magerezani, wengine kupelekwa uhamishoni, na wengine watatendewa kama watumwa. Kadiri Roho wa Mungu anavyoendelea kuondolewa kutoka kwa watu kutakuwa na mambo ya ajabu yatakayoendelea. Moyo wa mwanadamu naweza kuwa na ukatili sana ikiwa upendo na hofu ya Mungu vimeondolewa. TK 366.3