Kadiri Sabato itakavyozidi kuwa mada kuu iletayo utata kwa jamii ya Wakristo, itaamriwa kwamba wale wachache wanaopingana kanisa na serikali hawapaswi kuvumiliwa, kwamba ni heri wao kuteseka kuliko taifa lote kuingia katika machafuko na vurugu. Hoja hiyo hiyo ilitolewa dhidi ya Kristo,“wala hamfikiri ya kwamba yafaa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima.” Yohana 11:50. Hoja hii itaonekana kuwa ni hitimisho; hatimaye amri itatolewa dhidi ya wale wote wanaoiheshimu Sabato ya amri ya nne, kiwashutumu ni wakosaji na kuwapa watu uhuru baada ya muda fulani kuwaua. Ukatoliki wa ulimwengu wa zamani na Uprotestanti ulioasi katika ulimwengu wa kisasa utatekeleza jukumu lile lile. Kisha watu wa Mungu wataingizwa katika hayo matukio ya mateso ambayo yanajulikana kama “taabu ya Yakobo.”-Yeremia 30:5-7. TK 371.2
Usiku wa uchungu kwa Yakobo, alipokesha katika maombi ili aokolewe na mikono ya Esau; (Mwanzo 32:24-30) unawakilisha uzoefu wa watu wa Mungu wakati wa taabu. Kwa sababu ya uongo aliousema ili apate baraka za baba yake zilizokuwa zimekusudiwa kwa ajili ya Esau, Yakobo alitoroka, ikiogopa vitisho vikali vya kaka yake. Baada ya kukaa miaka kama mkimbizi, alipanga kurudi nyumbani kwao. Alipofika mpakani alijawa na hofu kutokana na taarifa za kuja kwa Esau, ambaye bila shaka angelipiza kisasi. Tumaini pekee la Yakobo lilikuwa ni rehema za Mungu; ulinzi wake pekee ulipaswa kuwa ni maombi. TK 371.3
Akiwa yeye na Mungu, aliungama dhambi zake kwa unyenyekevu. Zahama ilikuwa imemfikia katika maisha yake. Aliendelea kuomba katika gizani. Ghafla mkono uliwekwa begani mwake. Alidhani adui alikuwa akiutafuta uhai wake. Kwa nguvu zote akiwa amekata tamaa alipambana na adui yake. Kulipoanza kupambazuka, malaika alitumia nguvu zisizokuwa za kawaida. Yakobo alionekana kuishiwa nguvu na akaanguka, akiomba na kulia, shingoni mwa mpinzani wake wa ajabu. Ndipo alitambua kuwa alikuwa akipambana na malaika wa agano. Kwa muda mrefu alikuwa amevumilia kuugua kwa nafsi kulikotokana na dhambi yake; sasa alipaswa kuwa na uhakika kuwa ilikuwa imesamehewa. Malaika akamwambia, “Niache, niende, maana kunapambazuka” lakini Yakobo akamwambia “sikuachi usiponibariki” Yakobo aliungama kutostahili kwake, akatumainia rehema za Mungu mwenye kushika agano. Kwa njia ya toba na kujisalimisha, huyu mdhambi apatikanaye na mauti alimshinda Mwenye enzi wa mbinguni. TK 372.1
Shetani alikuwa amemshitaki Yakobo mbele za Mungu kwa sababu ya dhambi yake, akamshawishi Esau aende kupambana naye. Katika usiku wa mieleka wa mzee Yakobo, Shetani alikusudia kumkatisha tamaa na kuvunja tumaini lake kwa Mungu. Alikuwa amefikishwa karibu na hali ya kuvunjika moyo; lakini alikuwa amefanya toba ya dhati ya dhambi yake na kumng’ang’ania malaika akiomba kwa bidii na machozi hadi akashinda. TK 372.2
Namna Shetani alivyomshtaki Yakobo, ndivyo atakavyo yaleta mashtaka yake dhidi ya watu wa Mungu. Anazifahamu vizuri dhambi ambazo alizitumia kuwashawishi wazitende na anatangaza kwamba kwa kufuata haki, Bwana hawezi kuwasamehe dhambi zao bado amuangamize yeye pamoja na malaika zake. Anadai kuwa wakabidhiwe mikononi mwake ili waangamizwe. TK 372.3
Bwana atamruhusu ili awajaribu kwa kiwango cha juu. Ujasiri wao kwa Mungu, imani yao itajaribiwa vikali. Kadiri watakavyokumbuka maisha yao yaliyopita, matumaini yao yatazama, kwa sababu katika maisha yao yote wataweza kuona mema machache. Shetani atajitahidi kuwatishia ka dhana kwamba hakuna matumaini katika mashtaka yao. Kwa njia hiyo atakusudia kuharibu imai yao na kwamba watashawishika kwa majaribu yake na kugeuka na kuuacha uaminifu wao kwa Mungu. TK 372.4