Go to full page →

Mungu Analaumiwa Kwa Sababu ya Maumivu TK 373

Lakini uchungu ambao watu wa Mungu wataupata hautakuwa hofu ya mateso. Watahofu kuwa kwa sababu ya makosa yao fulani, ahadi ya Mwokozi: “Mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.”- Ufunuo 3:10, haitatimia kwao.. Wakidhihirisha kutostahili kwao kwa sababu ya upungufu katika tabia zao, jina takatifu la Mungu litatukanwa. TK 373.1

Wataikumbuka toba ya zamani juu ya dhambi zao nyingi na wataomba ahadi ya mwokozi: “Au azishike nguvu zangu, Afanye amani nami; Naam, afanye amani nami.” Isaya 27:5. Hata kama watasumbuliwa na mateso, msongo na huzuni; hawataacha kuomba. Watamshika Mungu kama Yakobo alivyomshika malaika, na lugha ya roho zao itakuwa “Sitakuachia uende, mpaka unibariki.” TK 373.2