Katika kipindi cha taabu, kama watu wa Mungu watakuwa na dhambi ambazo hawakutubu, ambazo zitatokea mbele yao wakati wakiwa katika ile hofu na uchungu; kwa hakika watashindwa. Kukata tamaa kutaondoa imani yao, na hawataweza kumsihi Mungu awaokoe. Lakini hawatakuwa na makosa yoyote yatakayohitaji kufunuliwa. Dhambi zao zitakuwa zimetangulia kwenye hukumu na kuondolewa, na hawataweza kuzikumbuka. TK 373.3
Katika kushughulika na Yakobo, Bwana ameonesha kwamba hawezi kuvumilia uovu. Wale wote wanaotoa udhuru au kuzificha dhambi zao na kuruhusu ziendelee kuwepo kwenye vitabu vya mbinguni bila kutubu na kusamehewa wanashindwa na Shetani. Kwa kadiri wanavyozidi kupanda vyeo, ndivyo adui yao anavyozidi kuwashinda. Wanaochelewa kufanya maandalizi hivi sasa hawatapata nafasi hiyo wakati wa taabu. Hali ya watu wote kama hao haina matumaini. TK 373.4
Historia ya Yakobo ni uhakika pia kwamba Mungu hatawatupa wale ambao baada ya kudanganyika dhambini, wameamua kurudi kwake kwa toba ya kweli. Mungu atatuma malaika kuwafariji wakati wa shida. Jicho la Bwana lipo juu ya watu wake. Miali ya moto wa tanuru inaonekana karibu itawaangamiza, lakini msafishaji atawatoa wakiwa kama dhahabu iliyojaribiwa motoni. TK 373.5