Nabii Isaya alisema: “Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, walizojifanyia ili kuziabudu, kwa fuko na popo; ili aingie ndani ya pango za majabali, na ndani ya tundu za miamba iliyopasuka, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.” Isaya 2:20,21. TK 382.4
Wale waliotoa vyote kwa ajili ya Kristo sasa watakuwa salama. Mbele za ulimwengu na mbele za kifo watakuwa wamedhihirisha uaminifu wao kwake aliyewafia. Nyuso zao ambazo muda mfupi kabla zilikuwa zimepauka na zisizopendeza, sasa zitang’aa kwa mshangao. Watapaza sauti katika wimbo wa ushindi: “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari“Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.” Zaburi 46:1-3. TK 383.1
Wakati maneno haya ya watakatifu yatakapokuwa yanapaa kwa Mungu, utukufu wa jiji la mbinguni utashuka kutoka kwenye malango yaliyo wazi. Kisha hapo utatokeza kutoka angani mkono ambao umebeba mbao mbili za mawe. Ile sheria takatifu, iliyotangazwa kutoka Sinai, sasa itafunuliwa kuwa kanuni ya hukumu. Maneno yatakuwa wazi kabisa kiasi cha watu wote kuweza kuyasoma. Kumbukumbu zitahuishwa. Giza la imani potovu na uasi litaondolewa katika kila moyo. TK 383.2
Haiwezekani kuelezea utisho na kukatishwa tamaa kwa wale walioikanyaga sheria ya Mungu. Ili kuifurahisha Dunia, waliweka sheria za Mungu pembeni na kuwafudisha watu uasi. Sasa watahukumiwa na sheria ileile walioidharau. Watajiona kuwa hawana udhuru. Adui wa sheria ya Mungu watapata ufahamu mpya kuhusu kweli na wajibu. Sasa wakiwa wamechelewa ndipo wataona kwamba Sabato ni muhuri wa Mungu aliye hai. Wakiwa wamechelewa watauona msingi wa mchanga ambao walikuwa wakijenga juu yake. Wamekuwa wakipigana dhidi ya Mungu. Walimu wa dini walikuwa wakiwaongoza watu Jehannamu huku wakidai kuwaongoza kwenda Paradiso. Ni kubwa kiasi gani jukumu la watu wanaofanya kazi katika ofisi takatifu, Ni ya kutisha jinsi gani matokeo yao ya kutokuwa waaminifu .! TK 383.3