Wakati ulinzi wa sheria za wanadamu utakapoondolewa kutoka kwa W wale ambao wanaiheshimu sheria ya Mungu, sambamba na hilo, katika nchi tofauti kutakuwa na harakati za kutaka kuwaangamiza. Kadiri wakati utakaotajwa kwenye sheria utakapokaribia, watu watapanga njama ili kufanya shambulio kubwa katika usiku mmoja litakalo nyamazisha upinzani na shutuma. TK 381.1
Watu wa Mungu baadhi yao wakiwa magerezani, misituni, na katika milima-wataomba ulinzi wa Mungu. Watu wenye silaha wakichochewa na malaika waovu watajiandaa kwa kazi ya mauaji. Sasa mnamo saa ya mwisho wa mateso, Mungu ataingilia kati: “Mtakuwa na wimbo kama vile wakati wa usiku, ishikwapo sikukuu takatifu, mtakuwa na furaha ya moyo kama vile mtu aendapo na filimbi katika mlima wa Bwana, aliye Mwamba wa Israeli. Naye Bwana atawasikizisha watu sauti yake ya utukufu, naye atawaonyesha jinsi mkono wake ushukavyo, na ghadhabu ya hasira yake, na mwako wa moto ulao, pamoja na dhoruba, na tufani, na mvua ya mawe ya barafu.” Isaya 30:29,30. TK 381.2
Makundi ya watu waovu yamekaribia kukimbilia mawindo yao, wakati giza nene, kuliko usiku, litakapoijilia nchi. Kisha upinde wa mvua utakuwa angani na utaonekana ukilizunguka kila kundi la wanaoomba. Makutano ya watu waliokasirika watakamatwa. Kusudi la ghadhabu yao limesahaulika. Wanashangaa ishara ya agano la Mungu na wanatamani kujificha mbali na mng’aro wake. TK 381.3
Watu wa Mungu watasikia sauti, ikisema, “tazama juu,” Kama Stefano, watatazama juu na kuuona utukufu wa Mungu na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. (Angalia Matendo 7:55,56.) Watatambua alama za kudhalilishwa kwake, na kulisikia ombi, “Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa.”Yohana 17:24. Sauti itasikika ikisema, “Wamekuja, watakatifu, pasipo maumivu, pasipo kunajisiwa! Wamelishika neno la subira yangu.” Usiku wa manane Mungu atadhihirisha uwezo wake kwa ukombozi kwa watu wake. Jua litatokeza likiwaka kwa nguvu zake. Kisha ishara na maajabu yatafuata. Kwa hofu kuu waovu wataangalia matukio, wakati huo wenye haki wakiangalia alama za ukombozi wao. Katikati ya mbingu zenye ghadhabu, angani kutatokea wingu lenye utukufii usioelezeka ambapo itasikika sauti ya Mungu, kama sauti ya maji mengi, ikisema, “Imekwisha!” Ufunuo 16:17. TK 381.4
Sauti hiyo itazitikisa mbingu na nchi. Kutakuwa na tetemeko kubwa, “ambalo tangu wanadamu kuwako juu ya nchi hapakuwa namna ile, jinsi lilivyokuwa kubwa tetemeko hilo.” Ufunuo 16:18. Mawe yaliyopasuliwa yatasambaa kila mahali. Bahari itachochewa na kughadhibika. Utasikika mvumo wa sauti ya kimbunga kama sauti ya maShetani. Uso wa dunia utapasukapasuka. Misingi yake itaonekana kutengeneza ufa.. Bandari ambazo zimegeuka na kuwa kama Sodoma kwa uovu zitamezwa na maji yenye hasira. “Babeli mkuu” ukakumbukwa mbele za Mungu, “kupewa kikombe cha mvinyo ya ghadhabu ya hasira yake.” Ufunuo 16:19. Mvua kuu ya mawe itafanya kazi yake ya uharibifu. Miji yenye kiburi itaangushwa chini. Majumba ya kifahari ambamo watu walitumia kwa anasa utajiri wao yatabomoka mbele ya macho yao. Kuta za gereza zitabomoka vipande vipande na watu wa Mungu watawekwa huru. TK 382.1
Makaburi yatafunguka, na “wengi wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele.” “na hao waliomchoma.” Wale waliombeza Kristo alipokuwa katika maumivu ya kufa, na wapinzani wakorofi wa ukweli watafufuliwa ili kuiona heshima watakayopewa waaminifu. Danieli 12:2; Ufunuo 1:7. TK 382.2
Radi kali zitaifunika dunia kwa miali ya moto. Zaidi ya ngurumo, sauti, za kushangaza na kutisha zitatangaza maangamizo ya waovu. Wale waliokuwa na majivuno na wasiokuwa watii, waliokuwa wakali kwa watu wa Mungu woanashika amri, sasa watatetemeka kwa hofu. Mapepo yatatetemeka wakati watu watakuwa wakiomba rehema. TK 382.3