Malaika wamewekwa katika vituo kuwalinda wale ambao wamelitunza neno la subira la Kristo. Watakuwa wameshuhudia matatizo na kuwasikia wakitoa maombi yao. Watasubiri kauli ya Kamanda wao ya kuwadaka kutoka kwenye hatari yao. Lakini itawabidi wasubiri kwa kitambo kidogo. Watu wa Mungu sharti wakinywee kikombe na wabatizwe kwa ule ubatizo. Mathayo 20:20-23. Lakini kwa sababu ya wateule muda wa mateso utafupishwa. Mwisho utafika haraka kuliko matarajio ya watu. TK 378.4
Japokuwa tamko kuu litakuwa limekwisha weka muda maalum ambapo washika sheria watauawa, adui zao katika baadhi ya matukio watawashambulia kuondoa uhai wao. Lakini hakuna atakayeweza kuwapita walinzi watakaokuwa wameizingira kila nafsi yenye uaminifu. Wengine katika jitihada zao za kutoroka mijini watateswa, lakini mapanga yatakayoinuliwa dhidi yao yatavunjika kama mabua. Wengine watalindwa na malaika watakaoonekana kama watu ya vita. TK 379.1
Katika vipindi vyote vya historia malaika wametekeleza majukumu muhimu katika mambo ya wanadamu. Wameukubali ukarimu waliotendwa katika nyumba za watu, wamekuwa viongozi kwa wasafiri wa usiku, wamefungua milango ya magereza na kuwaweka huru watumishi wa Bwana. Waliliondoa jiwe kwenye kaburi la Mwokozi. TK 379.2
Malaika huenda kwenye makusanyiko ya watu waovu, kama walivyoenda sodoma kujua ikiwa wamevuka ukomo wa uvumilivu wa Mungu. Kwa ajili ya watumishi wachache wanaomtumikia Mungu kwa uhalisi, anazuia majanga na kudumisha amani kwa watu wengi. Wenye dhambi wanafahamu kidogo sana kwamba inawapasa kushukuru kwa sababu ya maisha yao ambayo yanalindwa kwa sababu ya waaminifu wachache ambao wao wanafuraia kuwatesa. TK 379.3
Mara kwa mara katika mabaraza ya dunia hii, malaika wamekuwa wasemaji. Masikio ya kibinadamu yamesikiliza maombi yao, midomo ya kibinadamu imedhihaki mashauri yao. Wajumbe hawa wa mbinguni wamedhihirisha uwezo mkubwa na kuwasaidia wale wanaoteseka kuliko walinzi walio bora sana wa kibinadamu. Wameyashinda na kuuzuia maovu ambayo yangesababisha mateso makubwa kwa watu wa Mungu. TK 379.4
Kwa hamu kubwa, watu wa Mungu wanasubiria dalili ya mfalme wao ajaye. Kadiri watu wanaoishandana na Mungu wananavyoendelea kusihi mbele zake. mbingu zitang’aa kwa mapambazuko ya milele. Kama ilivyo sauti tamu ya nyimbo za malaika, ndivyo yatakavyokuwa maneno yatakayoingia katika sikio: “msaada unakuja.” Sauti ya Kristo itatoka kwenye malango yaliyo wazi: “Tazama, niko pamoja nanyi. Msiogope. Nimepigana vita kwa niaba yenu, na kwa jina langu ninyi ni zaidi ya washindi.” TK 379.5
Mwokozi mpendwa atatuma msaada wakati tutakapouhitaji. Wakati wa taabu utakuwa ni wakati wa mateso ya kutisha kwa watu wa Mungu, lakini kila muumini wa kweli ataona kwa imani upinde wa ahadi za Mungu ukimzunguka. “Nao waliokombolewa na Bwana watarejea, Watafika Sayuni, wakiimba; furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; watapata shangwe na furaha; huzuni na kuugua zitakimbia.” Isaya 51:11. TK 380.1
Kama damu ya mashahidi Wakristo ingemwagwa wakati huu, uaminifu wao usingekuwa ushuhuda wa kuwashawishi wengine kuhusu ukweli, kwa sababu moyo mkaidi unakuwa umeyakataa mawimbi ya rehema mpaka yamekoma kuja. Ikiwa wenye haki sasa wangeanguka mateka kwa maadui zao, huo ungekuwa ushindi wa mfalme wa giza. Kristo amesema: “Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita. Kwa maana, tazama, Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao.” Isaya 26:20, 21 TK 380.2
Kwa wale ambao watakuwa wamesubiri kwa uvumilivu ujio wa Bwana na wale ambao majina yao yameandikwa kwenye kitabu cha uzima, ukombozi wao utakuwa wenye utukufu. TK 380.3