Sasa baraza lilihitaji uwepo wa Mwanamatengenezo. Hatimaye mfalme aliridhika, na Luther aliitwa. Hati ya kuitwa kwenye shauri ilitolewa pamoja na hati ya hakikisho la usalama wake. Hati hizi zilipelekwa huko Wittenberg kupitia kwa Mjumbe aliyepewa jukumu la kumpeleka Luther kwenye mji wa Worms. TK 97.2
Marafiki wa Luther walizijua chuki zisizo na sababu na uadui dhidi yake, na hivyo walipata hofu kuwa uhakikisho wa usalama wake haungeheshimiwa. Yeye alijibu: “Kristo atanipatia Roho wake ili niwashinde hawa watumishi wa upotovu. Ninawadharau wakati wa uhai wangu; nitapata ushindi dhidi yao kwa njia ya kifo changu. Wapo Worms wakishughulika kwa bidii juu ya kunilazimisha nikanushe; na hivi ndivyo nitakavyokanusha: Hapo kabla nilisema kuwa Papa ni wakili Wakristo; na sasa ninatangaza kuwa yeye ni adui wa Bwana na ni mtume wa Ibilisi.” 70Ibid., ch. 6. TK 97.3
Zaidi ya mjumbe wa kifalme, marafiki watatu waliazimu kumsindikiza Luther. Moyo wa Melanchthon ulifiimwa kwenye moyo wa Luther, na alitamani kumfuata. Lakini, hakupata kibali. Mwanamatengenezo alisema: “Endapo sitarejea, na maadui zangu wakiniua, endelea kufundisha, na usimame imara katika kweli. Fanya kazi kwa niaba yangu...kama ukiwa hai wewe, kifo changu hakitakuwa na madhara makubwa. 71Ibid., ch. 7. TK 97.4
Mioyo ya watu ililemewa na ubashiri wa kuhuzunisha. Walijua kuwa Maandiko ya Luther yalishutumiwa huko Worms. Mjumbe, alihofia usalama wa Luther kwenye baraza na alimwuliza ikiwa angeendelea na safari. Alijibu kuwa: “Ingawa ninapigwa marufuku katika kila mji, nitaendelea.” 72Ibid. TK 98.1
Katika mji wa Erfurt, Luther alipitia mitaa ambayo mara nyingi alikuwa anaikatisha, alitembelea chumba chake kwenye nyumba ya watawa. Alifikiria juu ya masumbufu aliyoyapata alipokuwa anapatiwa nuru ambayo sasa ilikuwa inafurika katika Ujerumani yote. Aliombwa ahubiri. Jambo hilo hakuruhusiwa kufanya, lakini mjumbe alimpa ruhusa, na mtawa ambaye wakati fulani aliwekwa kuwa mfanyakazi wa kazi ngumu kwenye nyumba hiyo, sasa aliingia kwenye mimbara. TK 98.2
Watu walimsikiliza kwa umakini mkubwa. Mkate wa uzima ulimegwa kwa ile mioyo yenye njaa. Kristo aliinuliwa mbele yao kupita Papa, mabalozi, watawala na wafalme. Luther hakuongea chochote juu ya hali yake ya hatari kubwa. Alikuwa ameuficha ubinafsi wake katika Kristo. Alijificha nyuma ya Mtu wa Kalwari, akitafuta tu kumwasilisha Yesu kama Mkombozi wa mwenye dhambi. TK 98.3