Mfalme Ferdinand alikuwa amekataa kuwasikiliza Wakuu wa Kiprotestanti; lakini kwa kutaka kutuliza mafarakano yaliyokuwa yanavuruga ufalme wake, katika mwaka uliofuata baada ya Upinzani wa Spires, Charles V aliitisha mkutano wa kidini kule Augsburg. Alitangaza nia yake ya kuongoza kikao hicho mwenyewe. Viongozi wa Waprotestanti walialikwa kuhudhuria. TK 132.3
Madiwani walimsihi mbunge wa Saxony asiende kwenye mkutano huo: “Je, siyo kujihatarisha kwenda na kujifungia ndani ya kuta za mji na adui yako mwenye nguvu?” Lakini wengine kwa uadilifu walisema, “Hebu wakuu na wawe na ujasiri na Mungu kwa kuwatumia atainusuru kazi yake.” Luther alisema, “Mungu ni mwaminifu, hatatuacha.” 124Ibid. bk. 14, ch. 2. TK 132.4
Mbunge alianza safari kuelekea Augsburg. Wengi walikwenda huko na wenye nyuso zilizokuwa na huzuni na mioyo iliyokuwa na wasiwasi. Lakini Luther aliyekuwa amefuatana nao hadi Coburg, aliwatia shime imani yao kwa kuimba wimbo uliokuwa umetungwa kwenye safari hiyo, “Ngome Madhubuti ni Mungu Wetu.” Wengi wa waliokuwa na mioyo mizito walichangamshwa kwa sauti tamu iliyokuwa inatia moyo. TK 133.1
Wakuu waliokuwa wamefanya matengenezo walikuwa wamedhamiria kutoa tamko la maoni yao, likiwa na ushahidi kutoka katika Maandiko na kuyatoa katika baraza hilo. Jukumu la kuandaa tamko hilo liliwekwa mikononi mwa Luther, Melanchthon, na washirika wao. Ungamo hili lilikubaliwa na Waprotestanti na walikusanyika na kuambatanisha majina yao katika waraka huo. TK 133.2
Wanamatengenezo walikuwa makini kuhakikisha kuwa kusudio lao halichanganywi na masuala ya kisiasa. Wakuu hao Wakristo walipoendelea kuweka sahihi zao kwenye Ungamo hilo, Melanchthon aliingilia kati na kusema, “Wanaotakiwa kupendekeza mambo haya ni wanateolojia na wachungaji na mambo mengine tuziachie mamlaka za wenye nguvu wa dunia hii.” “La hasha!” mimi mniondoe humo. Nimedhamiria kwa ushupavu kufanya kile kilicho sahihi, pasipo kujisumbua mwenyewe juu ya taji yangu. Ninataka sana kumkiri Bwana. Kofia yangu ya ubunge na joho langu la ngozi si vya thamani kwangu kama msalaba wa Yesu Kristo.” Alijibu John wa Saxony. Alipokuwa anachukua Kalamu, mmoja kati ya wakuu hao alisema, “Niko tayari ...kuachana na mali na maisha yangu endapo heshima ya Bwana wangu Yesu Kristo itanitaka kufanya hivyo.” “Nitakuwa tayari kuwaacha watu wangu, vyeo na heshima zangu hata kuiacha nchi ya baba zangu na fimbo mkononi,” na akaendelea kusema, “kuliko kuyapokea mafundisho mengine yoyote kuliko yale yaliyo katika Ungamo.” 125Ibid. bk. 14, ch. 6. TK 133.3
Wakati uliokuwa umepangwa ulifika. Charles V akiwa amezungukwa na wabunge na wakuu alitoa nafasi kwa kuzungumza Wanamatengenezo Waprotestanti. Kwenye mkutano huo wa mwezi Agosti ukweli wa Injili uliwekwa wazi na makosa ya utawala wa Papa yalibainishwa. Siku hiyo ilitangazwa kuwa ni siku kuu kubwa kabisa ya Matengenezo, na moja ya siku tukufu sana katika historia ya Ukristo na wanadamu.” 126Ibid. bk. 14, ch. 7. TK 133.4
Mtawa wa Wittenberg alisimama mwenyewe kule Worms. Na mahali pake kwa sasa walikuwa wamesimama watu wakuu na wenye uwezo mkubwa kabisa katika himaya hiyo. “Nimefurahi kupita kawaida ya kwamba nimeendelea kuwa hai mpaka wakati huu muda ambao Kristo ametukuzwa na watu maarufu na wenye uwezo mkubwa, waliokiri imani katikati ya upinzani, na kwenye mkutano uliotukuka sana.” TK 134.1
Lile ambalo mfalme alizuia lisihubiriwe kutoka katika mimbari lilitangazwa kutoka ikulu; kile ambacho wengi walikiona kuwa hakikuwa kinafaa hata watumishi kukisikiliza; kilisikilizwa kwa mshangao na mabwana na wakuu wa ufalme. Wana wa wafalme na taji zao, walikuwa ndio wahubiri, na hotuba ilikuwa ni ukweli wa Mungu wa kifalme.” 127Ibid. Tangu nyakati za mitume kamwe haijafanyika kazi kubwa ama kikiri imani kulikokuwa kunavutia zaidi.” TK 134.2
Moja ya kanuni aliyoishikilia Luther kwa uthabiti na kuiendeleza ni kutotumia nguvu ya dola kusaidia kazi ya Matengenezo. Alifurahi kwa sababu Injili ilipopokelewa na wakuu katika ufalme; walipopendekeza kuunganisha nguvu kwa ajili ya ulinzi yeye alitangaza ya kuwa, “mafundisho ya Injili yatalindwa na Mungu peke yake... Kwa mtazamo wake, tahadhari zote za kisiasa zilizokuwa zimependekezwa zilikuwa zimesababishwa na hofu isiyo ya lazima na mashaka yanayotokana na dhambi.” 128D’Aubigne, London ed., bk. 10, ch. 14. TK 134.3
Baadaye alipokuwa anazungumzia muunganiko wa wakuu waliokuwa wamefanya matengenezo baada ya kufikiri kwa kina, Luther alisema ya kwamba, “silaha pekee katika vita hivi inabidi uwe “upanga wa Roho.” Alimwandikia mbunge wa Saksoni: “Kwa dhamiri zetu, sisi hatutaweza kuuidhinisha ushirikiano uliopendekezwa. Msalaba Wakristo ni lazima ubebwe. Mheshimiwa usiwe na hofu. Tutatenda mambo makubwa zaidi kwa maombi yetu kuliko kile watakachofanya maadui zetu wote kwa majivuno yao.” 129Ibid. bk. 14, ch. 1. TK 134.4
Kutoka mahali pa siri pa sala ilitokea nguvu ile iliyoutikisa ulimwengu wakati wa Matengenezo. Kule Augsburg, Luther, “hakupitisha siku bila kutoa wakfu angalau saa tatu kwa ajili ya maombi.” Kwenye mahali pa siri chumbani kwake, alikuwa anasikika akiumimina moyo wake kwa Mungu kwa maneno yaliyojaa “ibada, kicho na tumaini.” Alimwandikia Melanchthon akisema, “endapo jambo hili si la haki, achana nalo, na ikiwa kusudio hilo ni jema, kwa nini tushindwe kutimiza ahadi zake Yeye aliyetuagiza tulale bila hofu?” 130Ibid. bk. 14, ch. 6. Wanamatengenezo Waprotestanti walikuwa wamejenga juu ya Kristo. Milango ya kuzimu isingewashinda! TK 135.1