Kutangazwa kwa tarehe maalum ya kurudi kwa Kristo kulisababisha upinzani mkubwa kutoka kwa watu wengi wa matabaka yote; tangu mchungaji aliyekuwa madhabahuni hadi mwenye dhambi aliyekubuhu. Wengi walisema kuwa walikuwa hawapingi fundishao la ujio Wakristo; walichokuwa wanapinga ni ile tarehe maalumu. Lakini jicho la Mungu lionalo kila mahali lilikuwa linasoma mioyo yao. Walikuwa hawataki kusikia kuWakristo alikuwa anakuja kuuhukumu ulimwengu kwa haki. Matendo yao yasingestahimili uchunguzi wa Mungu asomaye mioyo, na hivyo walikuwa wanaogopa kukutana na Mungu wao. Kama ilivyokuwa kwa Wayahudi wakati wa ujio wa kwanza Wakristo, hawakuwa tayari kumkaribisha Yesu. Pamoja na kukataa kusikiliza hoja za wazi kutoka katika Biblia, walikuwa wanawadhihaki wale waliokuwa wanamtafuta Bwana. Shetani alimdhihaki Yesu kwamba watu wake walikuwa wanampenda kidogo sana kiasi kwamba walikuwa hawatamani kuonekana kwake. TK 235.1
“Hakuna aijuaye siku wala saa” ndiyo hoja iliyokuwa inatolewa na wapinzani wa imani ya ujio.Maandiko yanasema, “Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake.” Mathayo 24:36Maelezo ya wazi ya aya hii yalikuwa yanatolewa na wale waliokuwa wanamtafuta Bwana, na matumizi mabaya ya aya hiyo kwa upande wa wapinzani wao yalidhihirishwa. TK 235.2
Kauli moja ya Mwokozi haiwezi kutumika kuhafifisha nyingine. Japo hakuna mtu aijuaye siku wala saa ya kuja kwake, inatupasa kujua inapokaribia. Kukataa au kupuuzia kujua ujio wake unapokaribia ni hatari kwetu kama ilivyokuwa kutokujua kuwa Gharika ilikuwa imekaribia katika siku za Nuhu. Kristo alisema, “Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi,wala hutaijua saa nitakayokuja kwako.” Ufunuo. 3:3. TK 235.3
Paulo anawazungumzia wale waliolisikia onyo la Mwokozi: “Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana.” 1 Thesalonike 5:2-5. TK 235.4
Lakini wale waliokuwa wanatafuta udhuru wa kuukataa ukweli, waliziba masikio yao wasisikie maelezo haya, na maneno “Hakuna mtu aijuaye siku wala saa” yakaendelea kutamkwa na wenye kudhihaki na hata na wale waliokuwa wakidai kuwa watumishi Wakristo. Watu walipokuwa wanauliza njia ya wokovu, walimu wa dini walisimama katikati yao na ukweli kwa kulifasili vibaya Neno la Mungu. TK 236.1
Kwa kawaida wale waliokuwa watauwa zaidi katika makanisa walikuwa wa kwanza kuupokea ujumbe. Kila mahali ambapo watu walikuwa hawadhibitiwi na wachungaji, po pote walipokuwa wanaweza kulichunguza Neno la Mungu wao wenyewe, fundisho la ujio lilikuwa linahitaji kulinganishwa na Maandiko tu, ili kuthibitisha mamlaka yake kutoka kwa Mungu. TK 236.2
Wengi walipotezwa na waume zao, wake zao, wazazi wao, au watoto wao, na wakafanywa waamini kuwa ni dhambi hata kusikiliza “uzushi” kama ule uliokuwa unafundishwa na Waadventista. Malaika waliagizwa kuwalinda sana watu hawa, kwani nuru nyingine ilikuwa haijawaangazia kutoka kiti cha enzi cha Mungu. TK 236.3
Wale waliokuwa wameupokea ujumbe waliungojea ujio wa Mwokozi wao. Muda waliokuwa wanatarajia kukutana naye ulikuwa karibu. Waliikaribia saa hiyo kwa umakini mtulivu. Hakuna aliyepitia hali hiyo anayeweza kuusahau muda huo mzuri wa kungojea. Kwa majuma kadhaa kabla ya siku hiyo, shughuli za kidunia ziliwekwa kando. Waumini waaminifu waliipeleleza mioyo yao kana kwamba katika saa chache wasingeyaona tena mambo ya ulimwengu. Hawakuwa wanaandaa “mavazi ya kupaa nayo,” bali wote waliona hitaji la ushahidi wa ndani kwamba walikuwa tayari kukutana na Mwokozi. Mavazi meupe kwao ulikuwa usafi wa moyo—tabia zilizosafishwa kwa damu ya Kristo iletayo upatanisho. Kujipeleleza ndani ya moyo kunapaswa kuwepo miongoni mwa watu wa Mungu hata sasa. TK 236.4
Mungu alikuwa amekusudia kuwapima watu wake. Mkono wake ulificha kosa lililokuwa katika upigaji hesabu wa vipindi vya unabii. Muda waliokuwa wanautarajia [yaani, kwamba Kristo angekuja katika majira ya kuchipua ya mwaka 1844] ulipita, naye Kristo hakutokea. Wale waliokuwa wanamngojea Bwana wao walivunjika moyo kwa uchungu mkubwa. Hata hivyo Mungu alikuwa anaijaribu mioyo ya wale waliokuwa wanadai kuwa walikuwa wanangojea kuonekana kwake. Wengi walikuwa wamechochewa na hofu. Watu walisema kuwa hwakuwahi kuamini kuWakristo angekuja. Walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kudhihaki huzuni ya wale waumini wa kweli. Lakini Yesu pamoja na jeshi iote la mbinguni alikuwa anawaangalia kwa upendo na huruma wale waaminifu waliokuwa wamevunjika moyo. Kama pazia linalotenganisha ulimwengu usioonekana na ule unaoonekana lingeondolewa, malaika wangeonekana wakiwakaribia watu hawa wenye saburi na kuwakinga na kejeli za Shetani. TK 236.5